Rumafrica
ilitembelewa na mwimbaji maarufu sana Tanzania katika ofisi yetu iliyoko Afrikasana Sinza
hapa jijini Dar es Salaam
siku ya tarehe 12.01.2013. Mwimbaji huyu alieleza maisha yake ya Ukristo akiwa
katika makanisa ya Kikatoliki na baadae kuhamia katika makanisa ya
Kipentekosti. Pia alitueleza jinsi gani wazazi wake walivyomchulia alipoamua
kuachana na dini ya wazazi wake. Mwimbaji huyu hakuishia hapo pia alitueleza
kipaji chake kikubwa cha uimbaji alikipata akiwa na umri gani na vitu gani
vilimfanya apende kuimba na kucheza. Matatizo aliyoyapata akiwa katoliki na
matatizo anayoyapata akiwa Pentekosti
Utaweza kujua kwanini aliamua kuita albamu yake “Sambamba na Yesu”..Ni mengi utajua kuhusu mwimbaji huyu..naomba ufuatilie mahojiano haya:
Utaweza kujua kwanini aliamua kuita albamu yake “Sambamba na Yesu”..Ni mengi utajua kuhusu mwimbaji huyu..naomba ufuatilie mahojiano haya:
Gideon Tryphone Mutalemwa
RUMAFRICA: Bwana Yesu asifiwe…
GIDEON: Amen mtumishi wa Mungu.
RUMAFRICA: Karibu sana katika ofisi za Rumafrica.
GIDEON: Asante
sana,
nishakaribia.
RUMAFRICA: Tungependa kujua jina lako lililoko katika cheti chako cha
kuzaliwa.
kuzaliwa.
GIDEON: Ameni..Ninaitwa Gideon
Tryphone Mutalemwa.
RUMAFRICA: Unaweza kutuelezea kwa kifupi historia
ya huduma yako.
GIDEON: Nilianza huduma ya uimbaji tangia nilipokuwa mdogo sana.
Nakumbuka miaka ya 1992 au 1993, ndipo nilipoanza kuimba kwaya nikiwa katika mkoa wa Kagera, parokia ya Mugala katika kanisa la Katoliki. Nilikuwa naimba nikiwa chini ya Mapadre, nikawa nafundishwa jinsi ya kuimba na jinsi ya kucheza. Nikafundishwa jinsi ya kutumia piano na taratibu za muziki, nikafundishwa kutunga nyimbo. Wakati ulivyokuwa unaendelea nikawa mzuri sana katika muziki, na baadaye nikawachaguliwa kuwa “conductor” wa kwaya na Mungu hakuishia hapo akaniwezesha kuchaguliwa na kuwa mwalimu wa kwaya.
Nakumbuka miaka ya 1992 au 1993, ndipo nilipoanza kuimba kwaya nikiwa katika mkoa wa Kagera, parokia ya Mugala katika kanisa la Katoliki. Nilikuwa naimba nikiwa chini ya Mapadre, nikawa nafundishwa jinsi ya kuimba na jinsi ya kucheza. Nikafundishwa jinsi ya kutumia piano na taratibu za muziki, nikafundishwa kutunga nyimbo. Wakati ulivyokuwa unaendelea nikawa mzuri sana katika muziki, na baadaye nikawachaguliwa kuwa “conductor” wa kwaya na Mungu hakuishia hapo akaniwezesha kuchaguliwa na kuwa mwalimu wa kwaya.
Kwa ufupi nimeanza siku nyingi, na ninataka kusema ni kipaji kutoka kwa
Mungu, kwahiyo mpaka hapa nilipofikia namshukuru sana Mungu.
RUMAFRICA: Rumafrica ingependa kujua, wakati uko katika kanisa
Katoliki na wazazi wako walikuwa wanasali hapo?
GIDEON: Ahaaaa..Mwana wa Mungu kama
unavyojua, wazazi wanapokuzaa wanajua wakupeleke wapi pa kuabudu, kwahiyo
upande walipo na wanaposali ndio mahalia ambapo unatakiwa ukulie hapo. Kwahiyo
mpaka sasa naongea wazazi wangu ni Wakatoliki
Gideon T. Mutalemwa akisisitiza jambo.
RUMAFRICA: Kile kipaji chako cha uimbaji ulichokuwa nacho ukiwa
katika kanisa la Katoliki, ni mtu alikiona kutoka kwako au kuna mtu alikushauri
kuwa una kitu ndani yako na unatakiwa kukifanyia kazi?
GIDEON: Nikiwa
Roman Catholic, niseme niligundua mwenyewe
kwa kuwa nilipenda muziki. Kwanza mabali na kuwa kanisani, nikiwa
mitaani
nilikuwa napenda sana kusikiliza miziki ya kawaida
nikiwa pia kwenye maharusi, sherehe mbalimbali, nilikuwa napenda sana
kuhudhuria, nilikuwa napenda sana kucheza na kudansi. Sasa nikaona
naendelea kupenda kufanya hivyo. Kwahiyo niligundua kuwa nina hicho kitu
ndani
yangu.
RUMAFRICA: Ukiwa katika hali yako ya kupenda muziki kipindi
hicho..Kuna watu gani ulikuwa unawapenda sana
ambao ni wanamuziki na wakawa mchango katika kudumisha kipaji chako cha
uimbaji?
GIDEON: Kwa kipindi hicho kulikkuwa hakuna kitu kama cha kupenda mwimbaji Fulani, ila ilikuwa mtu
anapotunganga nyimbo, tuseme, Ndumbalo akitunga nyimbo na zikipigwa katika
Parokia na kupendwa, basi zilikuwa zikisambazwa katika Parokia zote.
Kipindi
hicho cha nyuma, mbali ya kuwa Mkatoliki pia nilikuwa nikipenda waimbaji kama Pepe Kale, Arusi Mabellee, Sakis, Franco na wengine wengi. Miziki Kama hiyo ikipigwa
nilikuwa nacheza. Sikujua maana ya miziki hiyo, ila nilikuwa naipenda sana na najisikia rah
asana.
RUMAFRICA: Ukiwa Roman Catholic, Mapadre walikuchuliaje na huduma
yako ya uimbaji na kucheza?
GIDEON: ahaaaa….Mapadre walinipenda, nilikuwa nao natumika
pale Alutareni, ninapiga chechezo, kupiga kengere na kutoa huduma zingine
alutare.
Namshukuru
Mungu, nilikuwa napata
muda wa kuhuduma alutareni na pia kupata muda wa kufanya mazoezi ya muziki.
RUMAFRICA: Wakati wewe ni mwalimu, wanafunzi wako walikuwa
wanakuchukuliaje?
GIDEON: Kwakeli kipindi hicho watu walishangaa sana kwasababu nilikuwa mdogo sana. Nikawa nafundisha watu ambao ni
wakubwa. Kwa kweli ilikuwa ni mshangao, ila kwa kuwa walikuwa wamenizoea katika
sherehe nilizokuwa na hudhuria kwa kuwaburudisha ilikuwa kwa upande mwingine ni
kawaida.
Kwahiyo
wenzangu walikuja kutambua mimi ni kitu Fulani ndani yangu.
Gideon Mutalewa akijaribu kueleza aliyopitia katika maisha yake.
RUMAFRICA: Kwa sasa hivi unapatika wapi?
GIDEON: Kwa sasa napatikana Dar es Salaam. Ni Mpendekosti halisi ambaye
ni mwimbaji wa nyimbo za injili na kwa
upande mwingine nafanya huduma ya APOSTOLIC.
Kwa sasa napatika katika kanisa la HUDUMA NA MAOMBEZI SALASALA, MBEZI BEACH
kwa mtumishi wa Mungu Nabii Flora Peter. Hapo kanisani natumika katika upande
wa Worship and Praise. Katika huduma ya uimbaji mimi ni Praise Leader na wakati
mwingine wakati nakuwa sihudumu hapo kanisani, ninatoka na kuelekea mikoani
kwaajili ya kumuimbia Bwana katika makongamano mbalimbali pamoja na kuhubiri.
Na zaidi nataka kuwajulisha kuwa huduma yangu hasa inalenga sana vijijini na huu ndio
mzigo mkubwa nilionao. Ninapenda kufika vijiji visivyoweza kufikika.
RUMAFRICA: Ni kitu gani kilikusababishia wewe kutoka kanisa la
katoliki na kuhamia Pentekosti?
GIDEONI: Ninaweza kukujibu kuwa ni neema ya Mungu, unajua
haya mambo. Katika suala la imani, tunapoingia katika suala la kuhofu, ni suala
tunalopa kwa Mungu au ni kwa neema. Kwahiyo siwezi kusema nilipo na umri wa
miaka 18 ndipo nikaamua...hapana!! Ila ni nasema Mungu anapomkuta mtu na
kugumsa, basi humchomoa kutoka mahali husika anapokuwa na kumpeleka mahali
Fulani kwa makusudi yake Mungu mwenyewe.
RUMAFRICA: Wakati unamia Pentekosti kutoka kanisa la Katoliki, wazazi
wako walikuwa bado wako Katoliki.
GIDEON: Wazai wangu walikuwa Roman Catholic na sasa bado
huko huko.
RUMAFRICA: Wazazi wako wanakuchukuliaje?
GIDEON: Aaaah….Mwanzoni walinichukulia vizuri, ninasema
hivyo kwasababu kuna maisha nilikuwa ninaishi kama kijana, starehe za dunia kama unavyojua, usumbufu nyumbani, leo umeondoka
asubuhi…umefanya kazi na labda umepita mitaa na ukanywa pombe. Kwahiyo ile pesa
yako ambayo unapata kazini badala ya kuitumia kuandaa “future” yako ya baadae,
unakuta inaishia kwenye maisha ya anasa zisizofaa.
Haikuwepo hofu, unafanya unachotaka kufanya. Hata kama kulikuwa na
mafundisho kanisani, lakini kulikuwa hakuna ile mkazo ya kwamba “Ukifanya hivi,
njia yako ni sehemu Fulani” kidogo hiyo hofu ilikuwa hamna, na hilo lazima tuwe wawazi
kuwa mtu ulikuwa “free” kufanya lolote.
Tukiwa tumefanya maovu, tulikuwa tunaenda kanisani, tunafanya KITUBIO na
baadae unaendelea na maisha ya kawaida.
Kwahiyo nilipookoka wazazi waliona kidogo mizigo wa matatizo umepungua
nyumbani. Wazazi wangu hawakulichukulia lile swala la kuhama dini kuwa mtoto
amehasi, kwani wazazi wangu walijua maisha ya walokole wanayoishi kwahiyo
wakaona afadhali aende kule (Aokoke).
RUMAFRICA: Ulipoingia sasa Pentekosti, ulianza moja kwa moja na
uimbaji au kunahuduma nyingine ulikuwa unafanya na baadae ukaanza huduma yako
ya uimbaji uliyotoka nayo Roman Catholic?
GIDEON: Mwana wa Mungu, baada ya kuwa Pentekosti, kwa
kweli sikuchelewa, na kama nilichelewa nakumbuka ni wiki mbili tu…Yaani kile
kitendo cha kupewa sala ya toba na kuanza kuingia kanisani na kupata yale
mafundisho ya mwanzoni, moja kwa moja niliivuta ile nguvu yangu niliyokuwa nayo
nafundisha na kuimba, nikajikuta na mimi natamani kusima katika kwaya kwani
nilitamani kuwaona wanavyoimba na kucheza.
Niliomba nafasi ya kuijiunga na nikakubaliwa, lakini kwasababu nilizoea
kuimba ile style ya Kikatoliki ya kuimba na kucheza taratibu. Kwahiyo ilichukwa
muda mwingi kuendana na style za Kipentekosti, ilichukua muda kama
mwezi mmoja. Na ninakumbuka nilimsumbua sana
mwalimu wangu wa kwaya, maana nyimbo ikitungwa ya kwenda haraka, mimi ninaenda
taratibu na ikitungwa ya haraka, mimi ninaenda taratibu.
Wanakwaya wenzangu na walimu walinipenda kwasababu nilikuwa na sauti
nzuri na ninauwezo wa kuimba, ila tu miondoko ya kucheza ilikuwa inanipa shida.
Nakumbuka kwa mara ya mwisho mwalimu alipata habari zangu na kunitaka
kuwa msaidizi wake nah ii ilifanyika ndani ya mwezi mmoja.
RUMAFRICA: Ulipojiunga na kwaya wenzako
walikuchukuliaje?
GIDEON: Kwa mara ya kwanza wenzangu walinishangaa sana kwasababu waliona moto umekuwa wa kasi sana. Kwasababu
nilipookoka ndani ya wiki mbili nikamuomba mchungaji niingie kundini (kwenye
kwaya), na mchungaji wangu alicheka sana.
Mchungaji akanipeleka kanisani akanitangaza na wanakwaya wakanipokea, na siku
za katikati ya wiki nikaenda kwenye mazoezi ya kuimba.
RUMAFRICA: Ni matatizo gani ulikuwa ukiyapata ukiwa katika kwaya?
GIDEON: Matatizo ni mengi na changamoto ni nyingi, maneno
yako mengi. Unajua unapokuwa katika kikundi kuna mamneno mengi, kudharauliana
na kusema mtu huyu ni bora kuliko mtu Fulani. Mambo hayo yapo na tunayazoea na
sisi ni binadamu tunatakiwa kusaidiana na kusamehana.
RUMAFRICA: Na ni kwanini hivi vitu vya kuoneana wivu vipo, wakati
tunajijua kuwa tumeokoka?
GIDEON: Niseme, binadamu kama
binadamu kuna zile ‘behaviors’ za kibinadamu huwezi kuzikwepa hata siku moja,
yaani zinahitaji neema ya Mungu kwa mtu kutambua ile “character” aliyonayo
kuiondoa.
Unatakiwa utambue ile tabia na uishughulikie mwenyewe. Tunakuta na
matatizo kama haya kwenye vikundi au kwa waimbakji kama
sisi, kwasabau ya hali ya kutojitambua kuwa wewe ni nani. Na cha pili ni
kutambua ni tabia gani iliyo ya ndani ambayo ni mbaya inayokufanya wewe usiwe
na hofu na lile baya.
Watumishi wanajitahidi kuomba lakini hatuwezi kupata majibu mazuri kama yule mtu unayemuombea hajajua tatizo lake.
Ninachotakka kusema ni mtu kuchukia yeye mwenyewe ile tabia aliyokuwa nayo.
Kwahiyo hatuwezi kuwakosa watu kama hao kama
hawajajiachilia wenyewe Mungu kushughulikia.
RUMAFRICA: Ni faida gani umezipata ukiwa katika
kwaya ya Kipentekosti?
GIDEON: Faida nilizopata ni kujifunza mengi,
1.
Kama nilivyosema kuwa kuna tabia
zilizotofautiana. Nikiwa Romani nilikuwa na tabia za kule na nilipoingia
Pentekosti nimepata tabia za Kipentekosti. Nilipoingia Pentekosti, nilidhani
ukishaokoka hakuna yale maneno ya kusemana vibaya, lakini nilipoingia
nikayakuta niliyoaacha Romani. Nikaja nikagundua kuwa kama
mwanadamu ili ujiweke huru ni wewe kujitambua na kusoma Neno la Mungu ili
likuweke huru na haya maovu yote.
2.
Faida nyingine ni ile kuzoea, ile style ya uimbaji na kucheza niliyokuwa natumia Romani Catholic ikabidi
ibadilike.
3.
Baada ya kuzoea ile style mpya ya uimbaji na kucheza (ya Kipentekosti),
nikaona sasa naweza kusimama mimi kama mimi na kumtumikia Mungu kwa njia ya
uimbaji na kucheza kama “SOLO ARTIST”.
RUMAFRICA: Wakati sasa unahama kutoka katika kwaya na
kuanza kusimama kama Solo Artist (mwimbaji wa kujitegemea), ulikuwa na uishi
Bukoba au Dar es Salaam?
GIDEON: Mhhh!!…anyway..niseme sikuwa nahama
kwaya na kuanza kuwa solo artist. Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nafundisha
nyimbo za Kiswahili nchi ya Uganda katika kituo kimoja kinaitwa Kaukuu Entebe
Road katika huduma inaitwa Mount Save Ministry, nakumbuaka mchungaji wangu
alikuwa anaitwa Deo, kwahiyo nilikuwa nikiimba halafu nikimaliza kuimba natoka
naenda studio, na kuna nyimbo nyingi niliziimba na sikuweza kuzitoa studio,
kwasababu nilikuwa naimba ili kujua ninauwezo gani wa kuimba. Ila nilitoa
nyimbo kama mbili na kuziachia radioni huko Karagwe na zikawa zinapigwa sana.Baada ya kutoka Uganda,
ndipo nilipokuja Dare s Salaam, nikaa kama
miaka miwili na baadae niakaanza kujipanga na kuona ninawezaje kuingia studio.
Gideon T. Mutalemwa akitafakari ya kumjibu mwandishi wa habari
RUMAFRICA: Vipi maisha yako ya muziki
ukiwa “Solo Artst?”
GIDEON: aaah..kwa kweli kwa sasa nina albamu yangu ambayo ni
Audio na Video. Albamu yangu inaitwa SAMBAMBA
NA YESU.
RUMAFRICA: Kwanini ulimamua jina la albamu yako kuitwa
jina hilo?
GIDEON: Nakumbuka Ilikuwa siku moja, tulikuwa
kanisani kwetu, kuna mtumishi mmoja alikuwa akihudumu pale kanisani kwetu na
badae alifariki. Alipofariki mchungaji akatuambie twende kwenye mkesha kwaajili
ya kuwatia moyo wafiwa, na usiku kikundi changu cha Praise kikawa kinaendesha
sifa mida ile ya usiku.
Sasa wakati naongoza sifa nikawa ninaimba mapambio. Yakaja maneno na
“melody” Nikajisikia kuguswa kutoka
katika nafsi yangu. Hata kama nilikuwa sijui yule mtumishi aliyekufa uhusiano
wake na Mungu, ila mimi kama mimi nilijua kuwa yule mtumishi ameondoka na
ameenda kwa Mungu moja kwa moja.
Ikanijia sauti palepale ninapoimba, mguso wa Mungu niliupata nikaona ya
kuwa hakika yume mtumishi ameenda mbele za Mungu pamoja na Kristo, ndipo
likanijia neno “Sambamba na Yesu” pamoja na “Melody”
Kwahiyo ilipokuja ile melody na ukiangalia nilikuwa na “beat” nilizokuwa
nimeziweka kati “flash”, nikaweza kuimba ile nyimbo muda huo huo usiku LIVE. Na
mpaka leo waimbaji wenzangu wa Praise Team hawakumbukagi kuwa hii nyimbo
ilipatika wapi, mahali gani na muda gani!!! Nakumbuka ile nyimbo nilipata usiku
kama saa saba au saa nanei usiku.
Nilikuwa naimba ile nyimbo kwa machozi mazito sana. Kwahiyo nikawa najua huyu mtumishi
ameondoka na Kristo..
Kwahiyo nikarudisha nyuma na kusema hata kama sio kufa, bado kuna yale
maisha tunatakiwa kuishi kama wana wa Mungu.
Au kama wanadamu kwa ujumla, tunatakiwa kuishi maisha pamoja na Kristo. Kila
kitu tunachotaka kufanya tufanye pamoja na Kristo, tunapoongea, tunapokula.
Ninakaona niimbe hii nyimbo na itaenda kugusa mioyo ya watu. Hata kama
kuna majaribu mengi tunakutana nayo.
Gideon T. Mutalemwa akiwa na furaha na amani wakati wa mahojiano na Rumafrica
RUMAFRICA: Albamu yako ina nyimbo
ngapi?
GIDEON: Ina nyimbo nane:
1.
Haleluaya
2.
Usalama uko kwa Yesu
3.
Utukuzwe
4.
Roho wa Bwana
5.
We Praise
6.
Nataka niseme na wewe
7.
Ni wewe peke yako
8.
Ntaya Yesu wange (Yesu wangu)- Hii ni nyimbo ya lugha ya Kihaya ambayo
ni Lugha yangu
RUMAFRICA: Katika albamu yako ni
nyimbo gani unaipenda?
GIDEON: Ha…!! Ninazipenda nyimbo nyingi, na
ninashindwa nichangue ni nyimbo gani…!!! Lakini naipenda sana “Sambamba na Yesu” kwasababu nakumbuka
nnipoimba studio wakati wa kurekodi, nilitokwa na machozi, nilijikuta naimba
mpaka “Producer” simuoni, na Producer alishakata kompyuta kwani muda umeisha,
mimi ndo kwanza naendelea kuimba na machozi yananitoka.
Gideon Mutalemwa ni mtumishi wa Mungu aliyejitoa kwa kazi ya Mungu
RUMAFRICA: Ni studio gani umefanya kazi yako ya audio na
video?
GIDEON: Audio nimefanya katika mazingira
magumu sana, na
nimefanya katika studio nyingi kwahiyo ninashindwa kusema nimefanyia studio
fulani. Ila amenifanyia mtu wa Mungu anaitwa Producer Itika, alikuwa akifanyia
katika studio mbalimbali. Na mara nyingi alikuwa akinipigia simu kuwa uko wapi,
naomba leo uje tukafanyie studio Fulani.
Video nimefanyia katika studio inaitwa MEDIA 55, bwana mmoja anaitwa
Delick au Mr. King.
RUMAFRICA: Ni matatizo gani uliyapata wakati wa uandaaji
wa albamu yako hii ambayo kwa sasa imekamilika?
GIDEON: Kwanza
ni mtaji wa kuingia studio, nauli ya kwenda studio na kurudi.
Pili, upande wa video ni jinsi gani ya kuwalipa na kuwaandalia chakula. Kuwasumbua wapiga picha kutoka Location moja na kwenda location nyingine.
Pili, upande wa video ni jinsi gani ya kuwalipa na kuwaandalia chakula. Kuwasumbua wapiga picha kutoka Location moja na kwenda location nyingine.
Tatu, kukosa watu wa ku-sponsor huduma yangu. Ila ninamshukuru Mungu kwa
kuwainua watu walioweza kunisaidia
Nne, kuna tatizo ambalo limekuwa likiniumiza sana nafsi yangu, ni kwamba kuna watu wengi
walikuw wameniahidi kuwa kazi yangu ni nzuri na watasimama na mimi, mtu
anakuahidi kuwa njoo sehemu Fulani au muda Fulani nitakutumia pesa, unapompigia
simu mara hapokei. Yaani unamwamini anapokutia moyo.
Nikaja kutambua kuna wapendwa waongo, walikuwa wanasema watakusaidia na hwakusaidii. Na mimi nilikuwa nawategemea kuwa na wana wa Mungu ambao nilikuwa nawaamini lakini sio waaminifu mbele yangu na mbele za Mungu.
Nikaja kutambua kuna wapendwa waongo, walikuwa wanasema watakusaidia na hwakusaidii. Na mimi nilikuwa nawategemea kuwa na wana wa Mungu ambao nilikuwa nawaamini lakini sio waaminifu mbele yangu na mbele za Mungu.
Lakini nimekuja kujua nimezidiwa na watu ambao sikutegemea, yaani mtu
yupo tu..mpo naye kanisani lakini apoona unaomba kitu, anaguswa na kukusaidia.
Kwahiyo nimetokea sana kutomtegemea sana kumtegemea mwanadamu
kwa kiukweli wanaangusha. Lakini Mungu anaweza kumtumia mtun yeyote
usiyemtarajia, kwahiyo Mungu ndiye anayenisaidia.
Nilikuwa naumia kwanini watu wa Mungu wananidanganya, lakini nikawa
nasaidia na watu mbali ambao hawana Mungu.
RUMAFRICA: Kutokana na hayo matatizo yako, nin unawambia
watu wote duniani?
GIDEON: Mimi ninamshukuru sana
Mungu kwani najua kuwa jaribu halimpati mtu kama
sio kiwango chake. Kwahiyo majribu yangu kama
ya kudanganywa na watumishi. Mtumishi anaponidanya mimi siwezim kuumia sana,
kwasababu sisi watumishi tunatumika kwa huyo tunayemtumikia, kwahiyo kama
tunayemtumikia yupo ambaye ni MUNGU wa vyote, ambaye ndiye anayemtumia yiule
asiyemwamini kwa kusaidia kazi yake, na wewe unayemjua Mungu unashindwa, ni
jambo la kujiuliza sana.
Ninachotaka kuuambia ulimwengu ni kwamba ile hali kidogo haikunipa
shida, nilijua kwamba anaponipitisha hapa ili mimi niendelee kujifunza kuwa
yeye anatengeneza njia.
Kwahiy wale wote walioniahidi kuwa wanisaidie na wakashindwa wasidhani nimekwazika,
labda ulikuwa sio mpango wa Mungu wao kunisaidia.
RUMAFRICA: Umeoa?
GIDEON: Nimeoa mke mmoja na nina mtoto mmoja
na mke wangu anaitwa Maryy na mama wa maombi, na ndiye anayenifanya niwe hivi
RUMAFRICA: Ni kitu umepanga kwa mwaka huu katika huduma
yako ya uimbaji?
GIDEON: Kwanza
albamu yangu itakuwa karibu na ni ndani ya
miezi miwili itakuwa sokoni.
Ninaomba watu wajiandae kuja kuipokea na kitu cha pili nimejipanga
kufanya uzinduzi ambao nitaanzia hapa Dar
es Salaam, katika kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya
Maombezi kwa Nabii Flora Peter. Na itakuwa tarehe 3.3.2013 kuanzia saa 8 mchana
mpaka saa 12 jioni baada ya ibada na hakutakuwa na kiingilio chochote.
Kama unavyosikia misemo yetu wanasema,
Mtenda Kwako Hutunzwa, ninawaomba, ndugu zangu wana kagera wote, tutiane moyo
katika huduma hii ya Mungu ambayo ninayo ndani yangu. Ninaomba ujue tumsifu
Mungu kwa lugha ya kikwetu.
Watanzania wote kwa ujumla ninawaomba sana, mimi ni kijana wenu, mje hiyo siku ili
tuweze kumtukuza Mungu na kumuabudu kwa pamoja.
Gideon Mutalemwa ni Baba mwenye mke mmoja na mtoto mmoja.
RUMAFRICA: Unawashauri nini waimbaji kama wewe?
GIDEON: Ninachotaka kuwaambia waimbaji na watu
wengine, ni kuhusiana na lugha inayotumika mitaani kwetu sisi waimbakji
inayoitwa WASANII.
Tumekuwa tukiitwa jina hilo
na waimbaji wengi walikuwa wakilikataa pasipokujua ya kwamba haiwapasi
walikatae.
Wanaitwa WASANII ni kwasababu, msanii ni mtu yeyote anayeweza ku-create
kitu chochote kama mtunzi, mchoraji na wengine
wengi katika ulimwengu na anaitwa yule ni MSANII.
Lakini wanatuita wasanii kwa maana nyingine, kwani wengi wanasema
wasanii wanataka sana
pesa. Hebu haya yote tuyaweke pembeni, ninachotaka kusema kama
Gideon, ninaomba tujitambue kuwa sisi ni watumishi wa Mungu. Kwa maaana katika
Biblia tunaposoma kuanzia Agano la Kale, tunakutana na habari ya kwamba,
“Walipokuwa Makuhani ndipo walipokuwa Walawi.” Walawi walikuwepo kwaajili ya
kuwabeba Makuhani. Kwahiyo tunapokuwa Walawi wasiopenda kupenda na
kushirikiana, kwa kweli kazi ya Mungu hatutaifanya.
Ili tulikatae hilo
jina la Wasanii, na tuitwe Watumishi wa Mungu, tunatakiwa kuwa na ushirikiano,
umoja na kupendana.
Kuna usemi mmoja unasema “Ma-underground”, hilo jina mara nyingi linasababisha kuwa na
maumivu makubwa ndani ya moyo wangu.
Kwa habari ya kutumika mbele za Mungu na Mungu anapomchagua mtu,
haangalii udogo wa mtu. Ninaposema hivyo, nina maanisha anaweza kuwa mdogo
kiumri au ni mdogo katika huduma yake na Mungu bado hajaanza kumuinua.
Kwahiyo wale walioko juu wasione sisi tulioko huku chini hatuweze kufanya chochote. Tunauwezo kufanya chochote na kuweza kuwasaidia hawa walioko juu.
Kwahiyo wale walioko juu wasione sisi tulioko huku chini hatuweze kufanya chochote. Tunauwezo kufanya chochote na kuweza kuwasaidia hawa walioko juu.
Ninachokiomba…hebu mtupende. Maana kuna watu wengi wanalalamika sana hapa mjini na tuachane na mikoani, wanasema, “Sisi
ma-underground tumekuwa tukitengewa, hatuhusishwi kwenye matamasha, na utakuta
wale wakubwa wamejitenga na wako peke yao.”
Yaaani hata mbele za Mungu sio haki na ninaimani Mungu hapendi.
Kwahiyo naomba tupendane, tushirikiane. Haata kama ni wadogo wanaweza
kumwasaidia watu.
Nakumbuaka daudi anaenda kupigana na Goliati, baba yake alimwambia avae
nguo za kiaskari aonekane askari ili akapigane. Lakini Daudi hakuweza kuvaa
yale mavazi, na akamwambia baba yake naomba niende na mavazi yangu; akayavua
yale magwanda akayaweka chini. Nimetoa huu mfano nikiwa na maana hii, kwamba
mimi naweza nikaonekana mdogo, kwa uwezo wangu siweze kufanya chochote na
ukashangaa nafanya makubwa.
Ninachowaomba ni kwamba, mtupe nafasi, na tunauwezo wa kushirikiana,
tukakaa pamoja, tukajenga tukawa pamoja.
Halafu kingine kuna chama cha CHAMUITA,
tumejiunga pale. Wapo waimbaji wakubwa na wapo waimbaji ambao ni wadogo. Kwa
ufahamu wangu ni kwamba na sisi ma-undaground tunatakiwa kuonekana kuwa tunafaa
katika uimbakji wa nyimbo za kumtumikia Mungu, ili tuwe karibu na dada na kaka
zetu ili tushirikiane kujenga mwili wa KRISTO.
Nembo ya CHAMUITA
Stella Joel akimwimbia Mungu katika kanisa la Nabii Flora
Albamu ya stella Joel upande wa nyuma
Ninachotaka kusema ni kwamba kuna vitu vingi tunaweza kusaidiana.
Gideoni leo ni underground lakini dada yangu, Stella Joel amenishirikisha
katika albamu yake ya “Hakuna mwanamke Mmbaya” katika albamu hiyo nimeimba nyimbo ya pili
inaitwa “Nakushukuru Mungu”
Mimi ni mdogo kimuziki, lakini dada yangu aliona ninakitu cha thamani
ambacho kinaweza kumfaidisha na tukashirikiana katika kuujenga mwili wa Kristo.
Ile nyimbo sijifagilii lakini nimeimba vizuri sana. Kwahiyo namshukuru Mungu kwani katika
waimbaji wote walioimba mle ni mastaa na mimi ndiye “underground” pekee.
Katika albamu hiyo kuna.
Katika albamu hiyo kuna.
1.
Rose Muhando
2.
Addo Novemba
3.
Stara Thomas
4.
Faraja Mutaboba
5.
Upendo Kilahiro
6.
Victor Mwana wa Aron
7.
Deogras Pius (DP)
8.
Lakini Gideon Mutalemwa yumo.
Tunaweza kuwa wadogo lakini tukawa na vitu
kutoka kwa Mungu ambavyo vinaweza kukusaidia na wewe mkubwa katika kuujenga
mwili wa Kristo.
MAHOJIANO YANAENDELEA
Unweza kuwasilia na mwimbaji huyu kwa
KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI MBEZI SALASALA-DAR ES SALAAM, EAST AFRICA.
KWA NABII FLORA PETER
Simu +255 719 697252 au +255 684 615423
Barua pepe: sambasambanayesu@gmail.com
Blogu: www.nabiiflora.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com
No comments:
Post a Comment