Sunday, January 13, 2013

GIDEON T. MUTALEMWA AELEZA JINSI ALIVYOHAMIA KANISA LA PENTEKOSTI KUTOKA KANISA LA KATOLIKI NA PIA JUU YA UZINDUZI WA ALBAMU YAKE YA KWANZA YA SAMBAMBA NA YESU


Rumafrica ilitembelewa na mwimbaji maarufu sana Tanzania katika ofisi yetu iliyoko Afrikasana Sinza hapa jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 12.01.2013. Mwimbaji huyu alieleza maisha yake ya Ukristo akiwa katika makanisa ya Kikatoliki na baadae kuhamia katika makanisa ya Kipentekosti. Pia alitueleza jinsi gani wazazi wake walivyomchulia alipoamua kuachana na dini ya wazazi wake. Mwimbaji huyu hakuishia hapo pia alitueleza kipaji chake kikubwa cha uimbaji alikipata akiwa na umri gani na vitu gani vilimfanya apende kuimba na kucheza. Matatizo aliyoyapata akiwa katoliki na matatizo anayoyapata akiwa Pentekosti

Utaweza kujua kwanini aliamua kuita albamu yake “Sambamba na Yesu”..Ni mengi utajua kuhusu mwimbaji huyu..naomba ufuatilie mahojiano haya:


 Gideon Tryphone Mutalemwa
RUMAFRICA:           Bwana Yesu asifiwe…
GIDEON:                   Amen mtumishi wa Mungu.
RUMAFRICA:           Karibu sana katika ofisi za Rumafrica.
GIDEON:                   Asante sana, nishakaribia.
RUMAFRICA:           Tungependa kujua jina lako lililoko katika cheti chako cha
kuzaliwa.
GIDEON:                   Ameni..Ninaitwa Gideon Tryphone Mutalemwa.
RUMAFRICA:           Unaweza kutuelezea kwa kifupi historia ya huduma yako.
GIDEON:                   Nilianza huduma ya uimbaji tangia nilipokuwa mdogo sana.
Nakumbuka miaka ya 1992 au 1993, ndipo nilipoanza kuimba kwaya nikiwa katika mkoa wa Kagera, parokia ya Mugala katika kanisa la Katoliki. Nilikuwa naimba nikiwa chini ya Mapadre, nikawa nafundishwa jinsi ya kuimba na jinsi ya kucheza. Nikafundishwa jinsi ya kutumia piano na taratibu za muziki, nikafundishwa kutunga nyimbo. Wakati ulivyokuwa unaendelea nikawa mzuri sana katika muziki, na baadaye nikawachaguliwa kuwa “conductor” wa kwaya na Mungu hakuishia hapo akaniwezesha kuchaguliwa na kuwa mwalimu wa kwaya.
Kwa ufupi nimeanza siku nyingi, na ninataka kusema ni kipaji kutoka kwa Mungu, kwahiyo mpaka hapa nilipofikia namshukuru sana Mungu.
RUMAFRICA:           Rumafrica ingependa kujua, wakati uko katika kanisa Katoliki na wazazi wako walikuwa wanasali hapo?
GIDEON:                   Ahaaaa..Mwana wa Mungu kama unavyojua, wazazi wanapokuzaa wanajua wakupeleke wapi pa kuabudu, kwahiyo upande walipo na wanaposali ndio mahalia ambapo unatakiwa ukulie hapo. Kwahiyo mpaka sasa naongea wazazi wangu ni Wakatoliki

 Gideon T. Mutalemwa akisisitiza jambo.RUMAFRICA:           Kile kipaji chako cha uimbaji ulichokuwa nacho ukiwa katika kanisa la Katoliki, ni mtu alikiona kutoka kwako au kuna mtu alikushauri kuwa una kitu ndani yako na unatakiwa kukifanyia kazi?
GIDEON:                   Nikiwa Roman Catholic, niseme niligundua mwenyewe kwa kuwa nilipenda muziki. Kwanza mabali na kuwa kanisani, nikiwa mitaani nilikuwa napenda sana kusikiliza miziki ya kawaida nikiwa pia kwenye maharusi, sherehe mbalimbali, nilikuwa napenda sana kuhudhuria, nilikuwa napenda sana kucheza na kudansi. Sasa nikaona naendelea kupenda kufanya hivyo. Kwahiyo niligundua kuwa nina hicho kitu ndani yangu.
RUMAFRICA:           Ukiwa katika hali yako ya kupenda muziki kipindi hicho..Kuna watu gani ulikuwa unawapenda sana ambao ni wanamuziki na wakawa mchango katika kudumisha kipaji chako cha uimbaji?
GIDEON:                   Kwa kipindi hicho kulikkuwa hakuna kitu kama cha kupenda mwimbaji Fulani, ila ilikuwa mtu anapotunganga nyimbo, tuseme, Ndumbalo akitunga nyimbo na zikipigwa katika Parokia na kupendwa, basi zilikuwa zikisambazwa katika Parokia zote.
                                    Kipindi hicho cha nyuma, mbali ya kuwa Mkatoliki pia nilikuwa nikipenda waimbaji kama Pepe Kale, Arusi Mabellee, Sakis, Franco  na wengine wengi. Miziki Kama hiyo ikipigwa nilikuwa nacheza. Sikujua maana ya miziki hiyo, ila nilikuwa naipenda sana na najisikia rah asana.
RUMAFRICA:           Ukiwa Roman Catholic, Mapadre walikuchuliaje na huduma yako ya uimbaji na kucheza?
GIDEON:                   ahaaaa….Mapadre walinipenda, nilikuwa nao natumika pale Alutareni, ninapiga chechezo, kupiga kengere na kutoa huduma zingine alutare.
                                    Namshukuru Mungu, nilikuwa napata muda wa kuhuduma alutareni na pia kupata muda wa kufanya mazoezi ya muziki.

RUMAFRICA:           Wakati wewe ni mwalimu, wanafunzi wako walikuwa wanakuchukuliaje?
GIDEON:                   Kwakeli kipindi hicho watu walishangaa sana kwasababu nilikuwa mdogo sana. Nikawa nafundisha watu ambao ni wakubwa. Kwa kweli ilikuwa ni mshangao, ila kwa kuwa walikuwa wamenizoea katika sherehe nilizokuwa na hudhuria kwa kuwaburudisha ilikuwa kwa upande mwingine ni kawaida.
                                    Kwahiyo wenzangu walikuja kutambua mimi ni kitu Fulani ndani yangu.


 Gideon Mutalewa akijaribu kueleza aliyopitia katika maisha yake.RUMAFRICA:           Kwa sasa hivi unapatika wapi?
GIDEON:                   Kwa sasa napatikana Dar es Salaam. Ni Mpendekosti halisi ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili na  kwa upande mwingine nafanya huduma ya APOSTOLIC.
Kwa sasa napatika katika kanisa la HUDUMA NA MAOMBEZI SALASALA, MBEZI BEACH kwa mtumishi wa Mungu Nabii Flora Peter. Hapo kanisani natumika katika upande wa Worship and Praise. Katika huduma ya uimbaji mimi ni Praise Leader na wakati mwingine wakati nakuwa sihudumu hapo kanisani, ninatoka na kuelekea mikoani kwaajili ya kumuimbia Bwana katika makongamano mbalimbali pamoja na kuhubiri.
Na zaidi nataka kuwajulisha kuwa huduma yangu hasa inalenga sana vijijini na huu ndio mzigo mkubwa nilionao. Ninapenda kufika vijiji visivyoweza kufikika.
RUMAFRICA:           Ni kitu gani kilikusababishia wewe kutoka kanisa la katoliki na kuhamia Pentekosti?
GIDEONI:                  Ninaweza kukujibu kuwa ni neema ya Mungu, unajua haya mambo. Katika suala la imani, tunapoingia katika suala la kuhofu, ni suala tunalopa kwa Mungu au ni kwa neema. Kwahiyo siwezi kusema nilipo na umri wa miaka 18 ndipo nikaamua...hapana!! Ila ni nasema Mungu anapomkuta mtu na kugumsa, basi humchomoa kutoka mahali husika anapokuwa na kumpeleka mahali Fulani kwa makusudi yake Mungu mwenyewe.
RUMAFRICA:           Wakati unamia Pentekosti kutoka kanisa la Katoliki, wazazi wako walikuwa bado wako Katoliki.
GIDEON:                   Wazai wangu walikuwa Roman Catholic na sasa bado huko huko.
RUMAFRICA:           Wazazi wako wanakuchukuliaje?
GIDEON:                   Aaaah….Mwanzoni walinichukulia vizuri, ninasema hivyo kwasababu kuna maisha nilikuwa ninaishi kama kijana, starehe za dunia kama unavyojua, usumbufu nyumbani, leo umeondoka asubuhi…umefanya kazi na labda umepita mitaa na ukanywa pombe. Kwahiyo ile pesa yako ambayo unapata kazini badala ya kuitumia kuandaa “future” yako ya baadae, unakuta inaishia kwenye maisha ya anasa zisizofaa.
Haikuwepo hofu, unafanya unachotaka kufanya. Hata kama kulikuwa na mafundisho kanisani, lakini kulikuwa hakuna ile mkazo ya kwamba “Ukifanya hivi, njia yako ni sehemu Fulani” kidogo hiyo hofu ilikuwa hamna, na hilo lazima tuwe wawazi kuwa mtu ulikuwa “free” kufanya lolote.
Tukiwa tumefanya maovu, tulikuwa tunaenda kanisani, tunafanya KITUBIO na baadae unaendelea na maisha ya kawaida.
Kwahiyo nilipookoka wazazi waliona kidogo mizigo wa matatizo umepungua nyumbani. Wazazi wangu hawakulichukulia lile swala la kuhama dini kuwa mtoto amehasi, kwani wazazi wangu walijua maisha ya walokole wanayoishi kwahiyo wakaona afadhali aende kule (Aokoke).
RUMAFRICA:           Ulipoingia sasa Pentekosti, ulianza moja kwa moja na uimbaji au kunahuduma nyingine ulikuwa unafanya na baadae ukaanza huduma yako ya uimbaji uliyotoka nayo Roman Catholic?
GIDEON:                   Mwana wa Mungu, baada ya kuwa Pentekosti, kwa kweli sikuchelewa, na kama nilichelewa nakumbuka ni wiki mbili tu…Yaani kile kitendo cha kupewa sala ya toba na kuanza kuingia kanisani na kupata yale mafundisho ya mwanzoni, moja kwa moja niliivuta ile nguvu yangu niliyokuwa nayo nafundisha na kuimba, nikajikuta na mimi natamani kusima katika kwaya kwani nilitamani kuwaona wanavyoimba na kucheza.
Niliomba nafasi ya kuijiunga na nikakubaliwa, lakini kwasababu nilizoea kuimba ile style ya Kikatoliki ya kuimba na kucheza taratibu. Kwahiyo ilichukwa muda mwingi kuendana na style za Kipentekosti, ilichukua muda kama mwezi mmoja. Na ninakumbuka nilimsumbua sana mwalimu wangu wa kwaya, maana nyimbo ikitungwa ya kwenda haraka, mimi ninaenda taratibu na ikitungwa ya haraka, mimi ninaenda taratibu.
Wanakwaya wenzangu na walimu walinipenda kwasababu nilikuwa na sauti nzuri na ninauwezo wa kuimba, ila tu miondoko ya kucheza ilikuwa inanipa shida.
Nakumbuka kwa mara ya mwisho mwalimu alipata habari zangu na kunitaka kuwa msaidizi wake nah ii ilifanyika ndani ya mwezi mmoja.


 Gideon Mutalemwa akimsikiliza mwandishi wa habari kwa makiniRUMAFRICA:           Ulipojiunga na kwaya wenzako walikuchukuliaje?
GIDEON:                   Kwa mara ya kwanza wenzangu walinishangaa sana kwasababu waliona moto umekuwa wa kasi sana. Kwasababu nilipookoka ndani ya wiki mbili nikamuomba mchungaji niingie kundini (kwenye kwaya), na mchungaji wangu alicheka sana. Mchungaji akanipeleka kanisani akanitangaza na wanakwaya wakanipokea, na siku za katikati ya wiki nikaenda kwenye mazoezi ya kuimba.
RUMAFRICA:           Ni matatizo gani ulikuwa ukiyapata ukiwa katika kwaya?
GIDEON:                   Matatizo ni mengi na changamoto ni nyingi, maneno yako mengi. Unajua unapokuwa katika kikundi kuna mamneno mengi, kudharauliana na kusema mtu huyu ni bora kuliko mtu Fulani. Mambo hayo yapo na tunayazoea na sisi ni binadamu tunatakiwa kusaidiana na kusamehana.
RUMAFRICA:           Na ni kwanini hivi vitu vya kuoneana wivu vipo, wakati tunajijua kuwa tumeokoka?
GIDEON:                   Niseme, binadamu kama binadamu kuna zile ‘behaviors’ za kibinadamu huwezi kuzikwepa hata siku moja, yaani zinahitaji neema ya Mungu kwa mtu kutambua ile “character” aliyonayo kuiondoa.
Unatakiwa utambue ile tabia na uishughulikie mwenyewe. Tunakuta na matatizo kama haya kwenye vikundi au kwa waimbakji kama sisi, kwasabau ya hali ya kutojitambua kuwa wewe ni nani. Na cha pili ni kutambua ni tabia gani iliyo ya ndani ambayo ni mbaya inayokufanya wewe usiwe na hofu na lile baya.
Watumishi wanajitahidi kuomba lakini hatuwezi kupata majibu mazuri kama yule mtu unayemuombea hajajua tatizo lake. Ninachotakka kusema ni mtu kuchukia yeye mwenyewe ile tabia aliyokuwa nayo.
Kwahiyo hatuwezi kuwakosa watu kama hao kama hawajajiachilia wenyewe Mungu kushughulikia.
RUMAFRICA:           Ni faida gani umezipata ukiwa katika kwaya ya Kipentekosti?
GIDEON:                   Faida nilizopata ni kujifunza mengi,
1.      Kama nilivyosema kuwa kuna tabia zilizotofautiana. Nikiwa Romani nilikuwa na tabia za kule na nilipoingia Pentekosti nimepata tabia za Kipentekosti. Nilipoingia Pentekosti, nilidhani ukishaokoka hakuna yale maneno ya kusemana vibaya, lakini nilipoingia nikayakuta niliyoaacha Romani. Nikaja nikagundua kuwa kama mwanadamu ili ujiweke huru ni wewe kujitambua na kusoma Neno la Mungu ili likuweke huru na haya maovu yote.

2.      Faida nyingine ni ile kuzoea, ile style ya uimbaji na kucheza  niliyokuwa natumia Romani Catholic ikabidi ibadilike.

3.      Baada ya kuzoea ile style mpya ya uimbaji na kucheza (ya Kipentekosti), nikaona sasa naweza kusimama mimi kama mimi na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na kucheza kama “SOLO ARTIST”.
RUMAFRICA:                       Wakati sasa unahama kutoka katika kwaya na kuanza kusimama kama Solo Artist (mwimbaji wa kujitegemea), ulikuwa na uishi Bukoba au Dar es Salaam?
GIDEON:                               Mhhh!!…anyway..niseme sikuwa nahama kwaya na kuanza kuwa solo artist. Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nafundisha nyimbo za Kiswahili nchi ya Uganda katika kituo kimoja kinaitwa Kaukuu Entebe Road katika huduma inaitwa Mount Save Ministry, nakumbuaka mchungaji wangu alikuwa anaitwa Deo, kwahiyo nilikuwa nikiimba halafu nikimaliza kuimba natoka naenda studio, na kuna nyimbo nyingi niliziimba na sikuweza kuzitoa studio, kwasababu nilikuwa naimba ili kujua ninauwezo gani wa kuimba. Ila nilitoa nyimbo kama mbili na kuziachia radioni huko Karagwe na zikawa zinapigwa sana.Baada ya kutoka Uganda, ndipo nilipokuja Dare s Salaam, nikaa kama miaka miwili na baadae niakaanza kujipanga na kuona ninawezaje kuingia studio.

 Gideon T. Mutalemwa akitafakari ya kumjibu mwandishi wa habariRUMAFRICA:                       Vipi maisha yako ya muziki ukiwa “Solo Artst?”

GIDEON:                               aaah..kwa kweli kwa sasa nina albamu yangu ambayo ni
                                                Audio na Video. Albamu yangu inaitwa SAMBAMBA
                                                NA YESU.
RUMAFRICA:                       Kwanini ulimamua jina la albamu yako kuitwa jina hilo?
GIDEON:                               Nakumbuka Ilikuwa siku moja, tulikuwa kanisani kwetu, kuna mtumishi mmoja alikuwa akihudumu pale kanisani kwetu na badae alifariki. Alipofariki mchungaji akatuambie twende kwenye mkesha kwaajili ya kuwatia moyo wafiwa, na usiku kikundi changu cha Praise kikawa kinaendesha sifa mida ile ya usiku.
Sasa wakati naongoza sifa nikawa ninaimba mapambio. Yakaja maneno na “melody”  Nikajisikia kuguswa kutoka katika nafsi yangu. Hata kama nilikuwa sijui yule mtumishi aliyekufa uhusiano wake na Mungu, ila mimi kama mimi nilijua kuwa yule mtumishi ameondoka na ameenda kwa Mungu moja kwa moja.
Ikanijia sauti palepale ninapoimba, mguso wa Mungu niliupata nikaona ya kuwa hakika yume mtumishi ameenda mbele za Mungu pamoja na Kristo, ndipo likanijia neno “Sambamba na Yesu” pamoja na “Melody”
Kwahiyo ilipokuja ile melody na ukiangalia nilikuwa na “beat” nilizokuwa nimeziweka kati “flash”, nikaweza kuimba ile nyimbo muda huo huo usiku LIVE. Na mpaka leo waimbaji wenzangu wa Praise Team hawakumbukagi kuwa hii nyimbo ilipatika wapi, mahali gani na muda gani!!! Nakumbuka ile nyimbo nilipata usiku kama saa saba au saa nanei usiku.
Nilikuwa naimba ile nyimbo kwa machozi mazito sana. Kwahiyo nikawa najua huyu mtumishi ameondoka na Kristo..
Kwahiyo nikarudisha nyuma na kusema hata kama sio kufa, bado kuna yale maisha tunatakiwa kuishi kama wana wa Mungu. Au kama wanadamu kwa ujumla, tunatakiwa kuishi maisha pamoja na Kristo. Kila kitu tunachotaka kufanya tufanye pamoja na Kristo, tunapoongea, tunapokula.
Ninakaona niimbe hii nyimbo na itaenda kugusa mioyo ya watu. Hata kama kuna majaribu mengi tunakutana nayo.

 Gideon T. Mutalemwa akiwa na furaha na amani wakati wa mahojiano na RumafricaRUMAFRICA:                       Albamu yako ina nyimbo ngapi?
GIDEON:                               Ina nyimbo nane:
1.      Haleluaya
2.      Usalama uko kwa Yesu
3.      Utukuzwe
4.      Roho wa Bwana
5.      We Praise
6.      Nataka niseme na wewe
7.      Ni wewe peke yako
8.      Ntaya Yesu wange (Yesu wangu)- Hii ni nyimbo ya lugha ya Kihaya ambayo ni Lugha yangu

RUMAFRICA:                       Katika albamu yako ni nyimbo gani unaipenda?
GIDEON:                               Ha…!! Ninazipenda nyimbo nyingi, na ninashindwa nichangue ni nyimbo gani…!!! Lakini naipenda sana “Sambamba na Yesu” kwasababu nakumbuka nnipoimba studio wakati wa kurekodi, nilitokwa na machozi, nilijikuta naimba mpaka “Producer” simuoni, na Producer alishakata kompyuta kwani muda umeisha, mimi ndo kwanza naendelea kuimba na machozi yananitoka.


Gideon Mutalemwa ni mtumishi wa Mungu aliyejitoa kwa kazi ya MunguRUMAFRICA:                       Ni studio gani umefanya kazi yako ya audio na video?
GIDEON:                               Audio nimefanya katika mazingira magumu sana, na nimefanya katika studio nyingi kwahiyo ninashindwa kusema nimefanyia studio fulani. Ila amenifanyia mtu wa Mungu anaitwa Producer Itika, alikuwa akifanyia katika studio mbalimbali. Na mara nyingi alikuwa akinipigia simu kuwa uko wapi, naomba leo uje tukafanyie studio Fulani.
Video nimefanyia katika studio inaitwa MEDIA 55, bwana mmoja anaitwa Delick au Mr. King.
RUMAFRICA:                       Ni matatizo gani uliyapata wakati wa uandaaji wa albamu yako hii ambayo kwa sasa imekamilika?
GIDEON:                               Kwanza ni mtaji wa kuingia studio, nauli ya kwenda studio na kurudi.

Pili, upande wa video ni jinsi gani ya kuwalipa na kuwaandalia chakula. Kuwasumbua wapiga picha kutoka Location moja na kwenda location nyingine.

Tatu, kukosa watu wa ku-sponsor huduma yangu. Ila ninamshukuru Mungu kwa kuwainua watu walioweza kunisaidia
Nne, kuna tatizo ambalo limekuwa likiniumiza sana nafsi yangu, ni kwamba kuna watu wengi walikuw wameniahidi kuwa kazi yangu ni nzuri na watasimama na mimi, mtu anakuahidi kuwa njoo sehemu Fulani au muda Fulani nitakutumia pesa, unapompigia simu mara hapokei. Yaani unamwamini anapokutia moyo.

Nikaja kutambua kuna wapendwa waongo, walikuwa wanasema watakusaidia na hwakusaidii. Na mimi nilikuwa nawategemea kuwa na wana wa Mungu ambao nilikuwa nawaamini lakini sio waaminifu mbele yangu na mbele za Mungu.
Lakini nimekuja kujua nimezidiwa na watu ambao sikutegemea, yaani mtu yupo tu..mpo naye kanisani lakini apoona unaomba kitu, anaguswa na kukusaidia.
Kwahiyo nimetokea sana kutomtegemea sana kumtegemea mwanadamu kwa kiukweli wanaangusha. Lakini Mungu anaweza kumtumia mtun yeyote usiyemtarajia, kwahiyo Mungu ndiye anayenisaidia.
Nilikuwa naumia kwanini watu wa Mungu wananidanganya, lakini nikawa nasaidia na watu mbali ambao hawana Mungu.

RUMAFRICA:                       Kutokana na hayo matatizo yako, nin unawambia watu wote duniani?
GIDEON:                               Mimi ninamshukuru sana Mungu kwani najua kuwa jaribu halimpati mtu kama sio kiwango chake. Kwahiyo majribu yangu kama ya kudanganywa na watumishi. Mtumishi anaponidanya mimi siwezim kuumia sana, kwasababu sisi watumishi tunatumika kwa huyo tunayemtumikia, kwahiyo kama tunayemtumikia yupo ambaye ni MUNGU wa vyote, ambaye ndiye anayemtumia yiule asiyemwamini kwa kusaidia kazi yake, na wewe unayemjua Mungu unashindwa, ni jambo la kujiuliza sana.
Ninachotaka kuuambia ulimwengu ni kwamba ile hali kidogo haikunipa shida, nilijua kwamba anaponipitisha hapa ili mimi niendelee kujifunza kuwa yeye anatengeneza njia.
Kwahiy wale wote walioniahidi kuwa wanisaidie na wakashindwa wasidhani nimekwazika, labda ulikuwa sio mpango wa Mungu wao kunisaidia.
RUMAFRICA:                       Umeoa?
GIDEON:                               Nimeoa mke mmoja na nina mtoto mmoja na mke wangu anaitwa Maryy na mama wa maombi, na ndiye anayenifanya niwe hivi
RUMAFRICA:                       Ni kitu umepanga kwa mwaka huu katika huduma yako ya uimbaji?
GIDEON:                               Kwanza albamu yangu itakuwa karibu na ni ndani ya  miezi miwili itakuwa sokoni.
Ninaomba watu wajiandae kuja kuipokea na kitu cha pili nimejipanga kufanya uzinduzi ambao nitaanzia hapa Dar es Salaam, katika kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi kwa Nabii Flora Peter. Na itakuwa tarehe 3.3.2013 kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 12 jioni baada ya ibada na hakutakuwa na kiingilio chochote.
Kama unavyosikia misemo yetu wanasema, Mtenda Kwako Hutunzwa, ninawaomba, ndugu zangu wana kagera wote, tutiane moyo katika huduma hii ya Mungu ambayo ninayo ndani yangu. Ninaomba ujue tumsifu Mungu kwa lugha ya kikwetu.
Watanzania wote kwa ujumla ninawaomba sana, mimi ni kijana wenu, mje hiyo siku ili tuweze kumtukuza Mungu na kumuabudu kwa pamoja.


Gideon Mutalemwa ni Baba mwenye mke mmoja na mtoto mmoja.RUMAFRICA:                       Unawashauri nini waimbaji kama wewe?
GIDEON:                               Ninachotaka kuwaambia waimbaji na watu wengine, ni kuhusiana na lugha inayotumika mitaani kwetu sisi waimbakji inayoitwa WASANII.
Tumekuwa tukiitwa jina hilo na waimbaji wengi walikuwa wakilikataa pasipokujua ya kwamba haiwapasi walikatae.
Wanaitwa WASANII ni kwasababu, msanii ni mtu yeyote anayeweza ku-create kitu chochote kama mtunzi, mchoraji na wengine wengi katika ulimwengu na anaitwa yule ni MSANII.
Lakini wanatuita wasanii kwa maana nyingine, kwani wengi wanasema wasanii wanataka sana pesa. Hebu haya yote tuyaweke pembeni, ninachotaka kusema kama Gideon, ninaomba tujitambue kuwa sisi ni watumishi wa Mungu. Kwa maaana katika Biblia tunaposoma kuanzia Agano la Kale, tunakutana na habari ya kwamba, “Walipokuwa Makuhani ndipo walipokuwa Walawi.” Walawi walikuwepo kwaajili ya kuwabeba Makuhani. Kwahiyo tunapokuwa Walawi wasiopenda kupenda na kushirikiana, kwa kweli kazi ya Mungu hatutaifanya.
Ili tulikatae hilo jina la Wasanii, na tuitwe Watumishi wa Mungu, tunatakiwa kuwa na ushirikiano, umoja na kupendana.
Kuna usemi mmoja unasema “Ma-underground”, hilo jina mara nyingi linasababisha kuwa na maumivu makubwa ndani ya moyo wangu.
Kwa habari ya kutumika mbele za Mungu na Mungu anapomchagua mtu, haangalii udogo wa mtu. Ninaposema hivyo, nina maanisha anaweza kuwa mdogo kiumri au ni mdogo katika huduma yake na Mungu bado hajaanza kumuinua.
Kwahiyo wale walioko juu wasione sisi tulioko huku chini hatuweze kufanya chochote. Tunauwezo kufanya chochote na kuweza kuwasaidia hawa walioko juu.
Ninachokiomba…hebu mtupende. Maana kuna watu wengi wanalalamika sana hapa mjini na tuachane na mikoani, wanasema, “Sisi ma-underground tumekuwa tukitengewa, hatuhusishwi kwenye matamasha, na utakuta wale wakubwa wamejitenga na wako peke yao.” Yaaani hata mbele za Mungu sio haki na ninaimani Mungu hapendi.
Kwahiyo naomba tupendane, tushirikiane. Haata kama ni wadogo wanaweza kumwasaidia watu.
Nakumbuaka daudi anaenda kupigana na Goliati, baba yake alimwambia avae nguo za kiaskari aonekane askari ili akapigane. Lakini Daudi hakuweza kuvaa yale mavazi, na akamwambia baba yake naomba niende na mavazi yangu; akayavua yale magwanda akayaweka chini. Nimetoa huu mfano nikiwa na maana hii, kwamba mimi naweza nikaonekana mdogo, kwa uwezo wangu siweze kufanya chochote na ukashangaa nafanya makubwa.
Ninachowaomba ni kwamba, mtupe nafasi, na tunauwezo wa kushirikiana, tukakaa pamoja, tukajenga tukawa pamoja.
  
Halafu kingine kuna chama cha CHAMUITA, tumejiunga pale. Wapo waimbaji wakubwa na wapo waimbaji ambao ni wadogo. Kwa ufahamu wangu ni kwamba na sisi ma-undaground tunatakiwa kuonekana kuwa tunafaa katika uimbakji wa nyimbo za kumtumikia Mungu, ili tuwe karibu na dada na kaka zetu ili tushirikiane kujenga mwili wa KRISTO.

Nembo ya CHAMUITA


Stella Joel akimwimbia Mungu katika kanisa la Nabii Flora
Albamu ya stella Joel upande wa nyumaNinachotaka kusema ni kwamba kuna vitu vingi tunaweza kusaidiana. Gideoni leo ni underground lakini dada yangu, Stella Joel amenishirikisha katika albamu yake ya “Hakuna mwanamke Mmbaya”  katika albamu hiyo nimeimba nyimbo ya pili inaitwa “Nakushukuru Mungu”
Mimi ni mdogo kimuziki, lakini dada yangu aliona ninakitu cha thamani ambacho kinaweza kumfaidisha na tukashirikiana katika kuujenga mwili wa Kristo. Ile nyimbo sijifagilii lakini nimeimba vizuri sana. Kwahiyo namshukuru Mungu kwani katika waimbaji wote walioimba mle ni mastaa na mimi ndiye “underground” pekee.
 


Katika albamu hiyo kuna.
1.      Rose Muhando
2.      Addo Novemba
3.      Stara Thomas
4.      Faraja Mutaboba
5.      Upendo Kilahiro
6.      Victor Mwana wa Aron
7.      Deogras Pius (DP)
8.      Lakini Gideon Mutalemwa yumo.
 Tunaweza kuwa wadogo lakini tukawa na vitu kutoka kwa Mungu ambavyo vinaweza kukusaidia na wewe mkubwa katika kuujenga mwili wa Kristo.MAHOJIANO YANAENDELEA
Unweza kuwasilia na mwimbaji huyu kwa
KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI MBEZI SALASALA-DAR ES SALAAM, EAST AFRICA.
KWA NABII FLORA PETER
 Simu +255 719 697252 au +255 684 615423
Barua pepe: sambasambanayesu@gmail.com
Blogu: www.nabiiflora.blogspot.com
            www.rumaafrica.blogspot.com

Sunday, August 26, 2012

MUIGIZAJI WA NIGERIA, TONTO DIKEH AFUNGULIWA KUPITIA EMMANUEL TV

Mtafsiri: Rulea Sanga

Muigizaji wa Nollywood, Toto Diken alisema katika mahojiana kutoka na kuokolewa kwa kuacha kuvuta sigara baada ya kuomba pamoja na TB Joshua kwa kupitia Emmanuel TV. Kutokana na Tonto ambaye alianza kuvuta sigara akiwa na umri wa miaka 13, alijiunga na Nabii TB Joshua katika maombi kwa kupitia Emmanuel TV na alipokea muujiza wake katika hali ambayo hakutegemea.

Aliliambia gazeti la Burudani la Nigeria, "Nilikuwa sivuti sigara mwenyewe, Nilikuwa naangalia kipindi katika TV cha Nabii TB Joshua na alikuwa amenyoosha mikono kwa watu huku akiwaobea. Huwa napenda kuangalia vipindi vyake katika Emmanuel TV. Alipokuwa akiomba, alisema, 'Nyoosha mikono yako katika T' nikanyoosha mikono yangu siku hiyo. Hasa nilikuwa nahitaji kitu kingine kutoka kwa Mungu, na sio kuvuta sigara kwasababu napenda kuvuta! Baada ya maombi nilikaa nilipokuwa nimekaa na nikajisikia kulala usingizi. "Baada ya maombi Tonto aliamka na akajisikia kuvuta kama kawaida yake, kitu cha kujua au kugundua ni kwamba hiyo ilikuwa ni tabia yake kwa muda wa miaka 14 ya kuvuta." Nilipoamka, nilichukua sigara na nikajisikia kama nimechanganyikiwa. Sikujigundua hata kuwa nimechukua hiyo sigara kwaajili ya kuvuta. Niliona kama sumu"


One of Nollywood’s rising actresses, Tonto Dikeh, revealed in an interview that she was delivered from an addiction to smoking through praying along with Prophet T.B. Joshua on Emmanuel TV. Glory be to God!According to Tonto, who started smoking at the tender age of 13, she joined Prophet T.B. Joshua to pray on Emmanuel TV and received the miracle in a way she never expected.
She told a Nigerian entertainment magazine, “I didn’t quit smoking by myself. I was watching a program on TV with Prophet T.B. Joshua and he was laying hands on people and praying for them. I love to watch his programs on Emmanuel TV. When he was praying, he said, ‘Lay your hands on the TV’ and I just laid my hands that day. I actually needed something else from God, not to quit smoking because I loved smoking! However, after praying I sat back and I think I slept off.”After the prayer, Tonto woke up and attempted to smoke as usual, only to discover that the very habit that had been part of her for 14 years suddenly became revolting. “When I woke up, I took a stick of cigarette and I felt crazy. I couldn’t even imagine that I took it up to smoke in the first place. It felt like poison!”

WAINJILISTI KUTOKA SCOAN KWA NABII T.B. JOSHUA KUINGIA TANZANIA

Mwandishi: Rulea Sanga

Watanzani tunaugeni mkubwa sana kutoka kwa Nabii TB Joshua. Hawa si wengine ni WAINJILISTI ambao wanakuja kutuhudumia Watanzania. Hii ni baraka tumepewa na Mungu kwa watu kama hawa kuingia nchini kwetu.

Tumekuwa tukiwaangalia katika Emmanuel TV kwa muda mrefu na tumekuwa tukitamani kuwaona uso kwa uso. Nisikuchoshe kwa maneno mengi mdau wangu, ngoja nikupe mchakato mzima 
Unatakiwa kufika Jumatatu 27.08.2012 saa moja katika ofisi za TB Joshua Dar es Salaam, na wale waliojiandikisha kwenda SCOAN Nigeria  waje pia na medical report zao eneo la Water Front jijini Dar es Salaam.
Wainjilisti watakutana na wale  waliojiandikisha kwenda SCOAN Nigeria siku ya Jumanne Diamond Jubilee.
Watanzania naomba tufike ili kupata ujumbe kutoka kwa watumishi wa Mungu. Mungu wangu awabariki.

Mimi kama blogger nawatia moyo kufika, kumbukeni na mimi nilipata muujiza wa kuonana na Nabii TB Joshua mwezi Aprili 2012


SCOAN-Nigeria

BBlogger Rulea Sanga nilipokuwa SCOAN Nigeriahttp://1.bp.blogspot.com/-QgCNSpoRH3U/TuTfotWYvqI/AAAAAAAAAd4/8MB1DG9Usa0/s1600/five_wise_men_SCOAN.jpg
Wise Men

Ndani ya Sinagogi

Kwaya ya SCOAN

Watu wengi wamepona kwa kupitia Emmanuel TV hasa pale unapogusa mkono wa Nabii TB Joshua ambao huunyosha katika screen yako

Tuesday, August 21, 2012

MTANZANIA ATOA USHUHUDA WAKE WA KUTOTOKWA NA DAMU BAADA YA KUANGALIA EMMANUEL TV YA TB JOSHUA

Mtafsiri: Blogger Rulea Sanga

Hapa kuna ushuhuda wa ajabu wa mtazamaji wa Emmanuel TV kutoka Tanzania ambaye alipokea ukombozi na uponyaji kwa kuangalia Emmanuel TV.

"Jina la Yesu lisifiwe! Ningependa kutoa shukrani zangu kwa timu nzima ya Emmanuel TV, Nabii T.B. Joshua na Wise Men kwa kazi ya Mungu na utayari wa kusaidia wengine"

Ninaushuhuda mkubwa sana ambao ningependa kushirikiana kwa ukombozi nilioupata kwa kuangalia Emmanuel TV! Ilikuwa siku ya Jumatatu 13/08/2012 wakati wa  "Live Service" , nilipokuwa naangalia Emmanuel TV wakati "Wise Men" walipokuwa wanawahudumia watu waliokusanyika pale. Nilimwona dada kutoka Zambabwe ambaye alikuwa na tatizo kama langu ambalo ni kutokwa na damu kutokana na roho ya mwanaume. Nilikuwa nikimuota huyu mwanaume katika ndoto zangu kwa miaka mingi sasa na nilikuwa nikitokwa na damu mfululizo kwa muda mrefu. Nilikuwa naogopa kwenda kulala kwasababu nilikuwa najua utakuwa usiku wa mateso na shida.

"Kwahiyo  "Wise Man" John Chi alipokuwa akimwombea yule mwanamke, imani yangu ikaanza kukua. Nilikuwa nalichukia hili pepo ambalo lilikuwa likinitesa mimi! Nilijisemesha mwenyewe, 'Kama huyu mwanamke atakombolewa, na mimi nitakuwa nimekombolewa.' Na alipokuwa anaombewa, nilianguka chini katika chumba changu! Siwezi kuelezea kitu gani kilinitokea lakini nguvu za Mungu zilinipiga katika mwili wangu. Na mwanamke wa Zimbabwe aliposema yuko huru kwa jina la Mungu, na mimi nikaanza kumshukuru Mungu kwa kukombolewa kwangu. Na mara alipokuwa amewekwa huru, na mimi nikawekwa huru!
"Kwa utukufu wa Mungu mpaka sasa, sitokwi tena na damu, na sioti tena ndoto mbaya tena. Nina furaha ya kutosha na amani katika moyo wangu. Jina la Yesu na liinuliwe na kutukuzwa milele na milele!" Aminia

Peace Gresmo, Tanzania
---------------------------------------------------------------------------

Spiritual Husband Exposed; Excessive Bleeding Stopped!

Here is a wonderful testimony from an Emmanuel TV viewer in Tanzania who received her deliverance and healing through watching Emmanuel TV:
“Praise the name of the living Jesus! I would like to extend my special thanks to the Emmanuel TV team, Prophet T.B. Joshua and also all the Wise Men for their commitment to God and readiness to serve others.
“I have a wonderful testimony to share about the deliverance I received through watching Emmanuel TV! Well, it was on Monday 13th August during the live service when I was watching Emmanuel TV as the wise men were ministering to the congregation. I saw a lady from Zimbabwe who had been tormented by exactly the same case as I had, which was a spiritual husband that caused excessive bleeding. I had been tormented by this strange man in my dreams for many years and had been bleeding continually for so long. I was always afraid of going to sleep because I know it would be a night of torment.
“So, when Wise Man John Chi was praying for her, faith began to rise in my heart. I was angry at this demon that was tormenting me! I said to myself, ‘If this lady will be delivered, I also will be delivered.’ As she was being prayed for, I suddenly fell down in my room! I can’t explain what happened but the power of God hit my body. As the lady from Zimbabwe was declared free by the man of God, I also started thanking God for my deliverance. As soon she was set free, I also was set free!
“To the glory of God, up to this moment, I am no longer bleeding and am not experiencing any bad dreams or nightmares anymore. There is so much joy and peace in my heart. May the name of Jesus be lifted on high and glorified forever and ever, amen!”
Peace Gresmo, Tanzania

Thursday, August 2, 2012

MAANA YA NAMBA 666


comments
Maandiko yanasema: ... siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo baba zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. (2 Petro 3:3-4).

Mtume Petro anatuambia hapa kwamba, watu watasema, “Kila siku mnasema, Yesu anakuja; Yesu anakuja. Yuko wapi? Mbona miaka inaenda tu. Msituzingue bwana!”
Je, hayo si ndiyo tunayoyasikia kila uchao? Mimi nimeshayasikia mara kadhaa. Naamini nawe pia umesikia dhihaka kama hizo.

Lakini maandiko yanasema kwamba: Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote waifikilie toba. (2 Petro 3:9).

Mungu anataka watu wote wamwamini Yesu na kupokea wokovu wa bure ambao Yeye aliulipia gharama kubwa ya uhai wake. Lakini nikwambie jambo: siku atakapotokea, hata kama kwa mtazamo wa kibinadamu ataonekana anachelewa, muda wote wa nyuma hautamfaidia kitu kamwe mtu ambaye hakumwamini Yeye ajaye! Cha msingi ni je, wakati huo atakukuta katika mkao gani kiimani?utakavyokuwa wakati huo ndicho kitakachoamua hatima yako ya milele!

Katika nyakati hizi tulizo nazo, dunia inajiandaa kuingia wakati wowote kwenye kipindi ufalme wa kuzimu wa moja kwa moja. Shetani atakuwa anatawala dunia moja kwa moja.

Kwa sasa, japo shetani yupo na anatenda kazi, lakini ni kwa kiwango cha chini. Maandiko yanasema: Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. (2 Wathesalonike 2:6-12).

Sasa huyu asi anapitia wapi? Biblia inasema kwamba: Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. (1 Timotheo 6:10).
Fedha ni kitu kizuri na muhimu sana katika maisha yetu. 

Lakini hapo pia ndipo penye nguvu na mlango wa kuzimu. Fedha au biashara au kwa túseme uchumi, vitahusika sana katika nyakati za mwisho za utawala wa shetani hapa duniani. Huu ni utawala ambao kimsingi maandalizi yake ni kama yameshakamilika.

Bwana Yesu ameshatupa taarifa juu ya kile kinachoitwa “chapa ya mnyama” ambayo watu watatakiwa kuwa nayo.
Imeandikwa: Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeyé aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. (Ufunuo 13:16-18).

Utendaji wa huyu asi umejikita kwenye kudhibiti fedha; uchumi wa dunia.

Namba 666 hadi sasa iko sehemu mbalimbali – hususani kwenye sekta ileile ya pesapesa, yaani biashara na uchumi.
Kama ninavyosema kwenye makala yangu mbalimbali, lengo kuu la shetani ni kuwasomba wanadamu wengi kadiri iwezekanavyo na kuwaingiza kuzimu, na hatimaye jehanamu ya motoni ambako yeye alishahukumiwa kuwa ndiko mahali pake pa milele.

Lakini ili aweze kuwapata wengi, lengo la kwanza lilikuwa ni kuwadanganya wanadamu ili wasimwamini Mungu – kazi ambayo ameshaifanya kwa mafanikio makubwa tu. Hata hivyo, kwa vile shauku yake bado ni kubwa mno, lengo lake la pili ni kuutawala ulimwengu kwa ukaribu na uwazi zaidi kuliko alivyofanya hadi sasa. Ndio maana hivi sasa kuna ajenda ya “new world order” ambayo iko mbioni kutekelezwa.
 Mpango huu una malengo kadhaa, yakiwamo yafuatayo:
 • Kuwa na serikali moja inayotawala dunia nzima; ambayo katika ndoto ya Nebukadreza iliyofasiriwa na Danieli, ni ule ufalme wa mwisho wa vidole vya chuma kilichochanganyika na udongo(Dan. 2:33).
 • Kuwa na uchumi mmoja duniani kote.
 • Kuwa na jeshi moja la dunia nzima.
 • Kuwa na dini moja duniani kote (huenda umeshasikia juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa sasa za kuanzisha dini hiyo, jambo ambalo linaungwa mkono na Umoja wa Mataifa). Hii ndiyo ambayo Bwana katika Ufunuo anaiita kahaba mkuu. (Ufu. 17:5).
Haya yote ni sehemu ya kutekeleza mpango wa kumleta kiongozi wa kishetani, yaani mpinga Kristo (yule asi), ambaye ataongoza dunia nzima.
Ili kuweza kudhibiti uchumi wa dunia yote pamoja na wanadamu watakaokuwapo wakati huo, inabidi uwepo mfumo wa kumfuatilia kila atakayekuwapo.

Kwa kuwa Bwana Yesu ameshatuambia kuwa hesabu ya jina la mnyama huyo ni 666, swali ni kuwa, je, kuna kitu kama hicho hivi sasa? Jibu ni ndio. Na ni mfumo ambao tunaukuta kulekule kwenye sekta ya biashara.

Mfumo huu umekuwapo duniani kwa muda mrefu sasa, huku ukiendelea kuboreshwa zaidi na zaidi kama ilivyo kwa teknolojia nyingine.

Chukua bidhaa mbalimbali – iwe ni gazeti, dawa ya meno, maji ya kunywa, mafuta ya kujipaka, sabuni ya kuogea, n.k., ukiangalia kwenye makasha au kwenye bidhaa zenyewe, utaona kitu kama hiki:
 
Hii ni kodi ya mistari (bar code). Kodi hii ina sehemu kuu mbili – sehemu ya kushoto na sehemu ya kulia. Sehemu hizo zimezungukwa na mistari mirefu zaidi ya mingine.

Namba unazoziona chini ya mchoro, upande wa kushoto, ni thamani ya mistari iliyo juu yake. Kila namba inawakilishwa na mistari miwili ya unene fulani na iliyotenganishwa na nafasi ya kiasi fulani. Mambo hayo matatu, yaani: mistari kuwa miwili, unene wa mistari na nafasi kati yake, hayabadiliki (suala la urefu halihusiki). Kwa hiyo, popote utakapoikuta mbili, mistari yake itakuwa na unene uleule na nafasi ileile kwa upande wa kushoto.
Hali kadhalika, kwa upande kulia nako namba zinakuwa na tabia hizo tatu lakini hazifanani na zile za kushoto. Tabia za kushoto ni za kushoto, na za kulia ni za kulia.
Lakini ningependa uangalie ile mistari mirefu mitatu. Ukiichunguza utaona kuwa inafanana kwa unene na nafasi kati yake. Hii inamaanisha kuwa inawakilisha namba ileile.

Sasa ili kujua hiyo ni namba gani, angalia kwenye kodi za bidhaa mbalimbali upande wa kulia (sio wa kushoto). Kisha angalia sehemu zote zenye 6. Chunguza mistari inayowakilishwa na 6. Utaona kuwa inafanana kabisa na ile iliyo mirefu. Hiyo itakuonyesha kuwa kumbe ile mistari mirefu ya katikati ni 666.

Kama nilivyodokeza hapo juu, hii ni sehemu mojawapo tu ambapo 666 inatumika.

Lakini tunachoweza kuona ni kwamba huu si mwonekano wa mwisho (final form) ya kile kitakachotumiwa na mpinga Kristo wakati wa kuitawala dunia.  

Chapa halisi ya mpinga Kristo, inadhaniwa na wengi kuwa itakuwa ni ‘electronic chip’ ndogo ambayo, kama anavyosema Bwana Yesu mwenyewe, itaweza kuwekwa kwenye mkono au usoni (hii inaonyesha kuwa ni kitu kitakachopandikizwa chini ya ngozi). Lakini bila shaka, kifaa hicho nacho kitakuwa na tabia zilezile za barcode; japo inaweza isifanane moja kwa moja na barcode za sasa.

Tabia mojawapo muhimu ya barcode ni kuwa inasomeka kielektroniki. Unapoenda kwenye supermarket, mhudumu huelekeza kwenye barcode kifaa kinachotoa namna ya mionzi fulani. Kwa sekunde moja kinasoma kila taarifa kuhusiana na bidhaa uliyochagua, kwa mfano bei yake, nk.

Lakini kwa sababu teknolojia ya chapa ya mnyama itakuwa ya juu zaidi, wale wadhibiti wa ulimwengu katika kipindi hicho, wataweza kufuatilia nyendo za kila mtu atakayekuwa amewekewa hicho kifaa.

Nihitimishe sehemu hii kwa kusema kwamba, barcodes zilizomo kwenye bidhaa madukani sasa hivi sio chapa halisi ya mpinga Kristo bali ilikuwa ni sehemu ya maandalizi ya teknolojia itakayotumika (ambayo tayari ipo kazini).

Lakini kama nilivyokueleza kwenye makala yangu ya mwisho kuhusu alama za kishetani (kama hukusoma unaweza kusoma hapa), shetani amekuwa kwenye harakati zake za kumharibu mwanadamu kwa miaka na miaka. Hizi barcodes zimekuwapo kwa muda mrefu, lakini  ni sehemu kabisa ya mpango wake huo wa uharibifu – japo wengi wanaweza kuzitazama kama maendeleo ya kawaida ya kiteknolojia yaliyoletwa na mwanadamu. Kumbuka siku zote, shetani ni kerubi afunikaye. (Ezekieli 28:14).

Katika sehemu ya pili na ya mwisho ya makala haya, nitakueleza jinsi ambavyo hivi sasa teknolojia imefikia juu zaidi na tayari watu wanaanza kupandikiziwa hizo ‘chip’. Usikose sehemu hiyo.

Rafiki, usilale. Shetani anakuja; na Yesu naye anakuja! Kama wewe ni mmoja wa wale wanaosema kuwa Biblia ni uongo; au kwamba Biblia imechakachuliwa, hakuna tena muda wamalumbano na mabishano. Fungua macho yako utazame upya sawasawa! Kila kitu kiko wazi sasa!

Yafuatayo ni maneno ya Bwana wa Mbingu na nchi: Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka  mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie. (Mathayo 5:18).
Kila alichokisema Mungu wa mbinguni kwenye Biblia NI LAZIMA kitimie! Na mengine ndiyo haya tunashuhudia mbele za macho yetu.

 Endelea kufuatilia pia masomo ninayoweka kwenye blog ya: www.injiliyakweli.blogspot.com na pia www.truthofgospel.blogspot.com. Ukiwa na maoni au chochote, unaweza pia kuniandikia kupitia

Tuesday, July 31, 2012

CHEMSHA BONGO NA BIBLE

Mtunzi wa Mtihani: Rulea Sanga

MITIHANI WA MWISHO WA MWEZI JULAI 2012 WA CHEMSHA BONGO NA BIBLE
Unatakiwa kujibu maswali yote kwa muda wa saa mbili na nusu. Tunaamini utazingatia hilo agizo kwasababu wewe ni mtumishi wa Mungu.

Majibu yako unaweza kunitumia katika email yangu rumatz2011@yahoo.com.

Angalia muda ulioanza kujibu kwa makini.

Kumbuka hapo ulipo unasimamiwa na Roho Mtakatifu kwahiyo huwezi kufanya jambo lakuangalizia.


Ukiangalizia Roho Mtakatifu na nguvu za Mungu zitakutoa katika chumba chako cha kufanyia mtihani.

Matokeo yako utatumiawa kwa email na utapewa na cheti cha kufanya mtihani.

Kila swali lina maksi 10

Jinsi ya kujibu: Unatakiwa kuchagua jibu sahihi na ukipata andika namba ya jibu na jibu lake kwa kuandika herufi kama ni A, B, au C. Na usiandike swali, wewe tutumie hiyo herufu na namba ya swali.


MASWALI YOTE NI YA KUCHAGUA

Chagua jibu sahihi;

 1. Kitu gani kilitokea wakati Yesu anabatizwa

               (a) Wingu jeusi

                (b) Tetemeko la ardhi

                (c) Mbingu za dunia zikamfunukia akaona Roho wa Mungu akishuka             
               kama hua, akija juu yake, na sauti kutoka juu ikisema, Huyu ni
               mwanagu mpendwa wangu, ninayependezwa naye

 2. Yesu alipopandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na ibilisi, alifunga kula siku ngapi?

                (a) kumi

                (b) Sita

                (c) Arobaini
 3.   (i) Yesu alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, akimsihi akisema, Bwana mtumishi wangu amelala, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu akamwambia,

                (a) Amini ameshapona

                (b) Nitakuja, nimponye

                (c) Nitakuja, nimuokoe na atapona.

  (ii) Yule akijibu akasema, Bwana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu, lakini sema neno na mtumishi wangu atapona. Yesu aliposikia hayo alistajabu akawambia wale waliomfuata

                (a) Amini na wambie sijaona imani kubwa kama hii kwa yeyote
               katika Israel

                (b) Amini na wambie sijaona imani kubwa kama hii kwa yeyote
               katika mkutano huu

                (c) Amini na wambie sijaona upendo kubwa kama huu kwa yeyote
               katika Israel

 4. (i) Kuna muujiza ambao Yesu aliufanya wa kuiongeza mikate na samaki ambapo wanafunzi wake walikula mpaka wakasaza. Ni mikate mingapi na samaki ngapi ambazo Yesu aliziombea kwa kutazama juu mbinguni kwa Mungu?

                (a) Mikate miwili na samaki watano

                (b) Samaki wawili na mikate mitano

                (c) Mkate mmoja na samaki waili

  (ii) Masazo yaliyobaki baada ya wanafunzi kula na kushiba ilijaa vikapu vingapi?

                (a) kumi na viwili

                (b) Kuma na saba

                (d) viwili

 5. Ni baada ya kufanya nini, Yesu aliwaambia, “Imeandikwa, nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala, bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi”.

                (a) Ni baada ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na
               kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
               waliokuwa wanauzia njiwa

                (b) Ni baada ya Yesu kuingia msikitini na kuona watu wakiuza na
               kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
               waliokuwa wanauzia njiwa

                (c) Ni kabla ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na
               kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
               waliokuwa wanauzia njiwa
 6. (i) Yuda alipoona ya kuwa Ysu amekwisha kuhukumiwa, alifanya nini?

                (a) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
               vipande thelathini na moja vya fedha

                (b) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
               vipande thelathini vya fedha

                (c) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
               vipande thelathini vya dhahabu

  (ii) Ni maneno gani Yuda alisema baada ya kurudisha vile vipande alivyopewa kwaajili ya kumsaliti Yesu?

                (a) Alisema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia
                (b) Alisema, Sijakosea nilipoisaliti damu isiyo na hatia
                (c) Alisema, Nalikosa nilipoisaliti damu iliyo na hatia

  (ii) Yuda baada ya kukimbia ndani ya hekalu kutokana na kumsaliti Yesu alifanya nini?

                (a) Alikimbia na kujinyonga

                (b) Alirudi na kumsujudia Yesu

                (c) Alihuzunika sana na kulia

 7. Baada ya kusikia kuwa Herode amekufa Misri, Yusufu, Yesu na Bikira Maria  walitoka Israel ni wapi walienda kuishi?

                (a) Nazareti

                (b) Misri

                (c) Marekani
 8. Taja majaribu matatu ambayo Yesu alijaribiwa na Ibilisi nyikani?

                (a) (i) Mawe yawe mikate

                    (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu

                    (iii) Kumsujudia Ibilisi

                (b) (i) Mchanga uwe mikate

                    (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha mlima

                    (iii) Kumsujudia Ibilisi

                (c) (i) Mawe yawe mikate

                    (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu

                    (iii) Kumsujudia Mfalme
 9. Yesu aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. Na tazama akaja mtu mwenye ukoma, akamsujudia akisema,

                (a) Bwana ukitaka unaweza kunitakasa

                (b) Bwana ukitaka waweza kunibariki

                (c) Bwana ukitaka waweza kunihurumia

 10. (i) Taja jina la mfalme aliyemfunga na kumtia Yohana Mbatizaji gereza?

                (a) Kayafa

                (b) Rulea Sanga

                (c) Mfalme Herode

  (ii) Kwani Yohana alifungwa gerezani?

                (a)  Yohana alimwambia sio halali kwa Herode kuwa na nduguye       
               Filipo awe mke wake na Herode.

                (b) Yohana alimwambia sio halali kwa Kayafa kuwa na nduguye
               Musa awe mke wake na Herode.

                (c) Majibu ya hapo juu sio sahihi

  (iii) Kwanini mfalme alipoona watu akaogopa kumuua Yohana Mbatizaji?

                (a)  Yohana alimwambia sio halali kwa Herode kuwa na nduguye
               Filipo awe mke wake na Herode.

                (b) Kwasababu watu walimuona Yohana Mbatizaji kama Nabii

                (c) Kwasababu watu walimuona Yohana Mbatizaji kama Mfalme

  (iv) Ni nani aliyecheza mbele ya Herode wakati wa sikuku yake ya kuzaliwa akampendeza Herode kwa uchezaji wake?

                (a) Binti Herode

                (b) Mjukuu wa Herode

                (c) Rafiki yake na Binti Herode

  (v) Ni nani alimshauri huyu mtu aliyecheza mbele ya mfalme Herode na mpaka Herode akakubali kutimiza kiapo chake cha kumpa chochote atakachoomba?

                (a) mama yake

                (b) Kaka yake

                (c) Rafiki yake

  (vi) Huyo aliyemfurahisha Herode kwa kucheza aliomba  nini apewe na huyo mfalme?

                (a) hakuomba chochote

                (b) aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji katika mfuko

                (c) aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji katika kombe

  (vii) Unafikiri Herode alifuarahia ilo ombi la huyu aliyecheza vizuri katika sikuku yake ya kuzaliwa? Na kama alifurahi au alisikitika ni kwanini?

                (a) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni aibu kwa watu waliokuwa
               nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika sikukuu yake

                (b) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni atakimbiwa na watu
               waliokuwa nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika
               sikukuu yake

                (c) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni si haki na ni uonevu  kwa
               watu waliokuwa nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika             
               sikukuu yake

  (viii) Baada ya kichwa cha Yohana Mbatizaji kukatwa na kukabidhiwa yule kijana alicheza vizuri mbele ya mfalme Herode, ni wapi alikipeleka hicho kichwa?

                (a) mama yake

                (b) Kaka yake

                (c) Rafiki yake


VANYASANGA POST TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...