Tuesday, July 31, 2012

CHEMSHA BONGO NA BIBLE

Mtunzi wa Mtihani: Rulea Sanga

MITIHANI WA MWISHO WA MWEZI JULAI 2012 WA CHEMSHA BONGO NA BIBLE
Unatakiwa kujibu maswali yote kwa muda wa saa mbili na nusu. Tunaamini utazingatia hilo agizo kwasababu wewe ni mtumishi wa Mungu.

Majibu yako unaweza kunitumia katika email yangu rumatz2011@yahoo.com.

Angalia muda ulioanza kujibu kwa makini.

Kumbuka hapo ulipo unasimamiwa na Roho Mtakatifu kwahiyo huwezi kufanya jambo lakuangalizia.


Ukiangalizia Roho Mtakatifu na nguvu za Mungu zitakutoa katika chumba chako cha kufanyia mtihani.

Matokeo yako utatumiawa kwa email na utapewa na cheti cha kufanya mtihani.

Kila swali lina maksi 10

Jinsi ya kujibu: Unatakiwa kuchagua jibu sahihi na ukipata andika namba ya jibu na jibu lake kwa kuandika herufi kama ni A, B, au C. Na usiandike swali, wewe tutumie hiyo herufu na namba ya swali.


MASWALI YOTE NI YA KUCHAGUA

Chagua jibu sahihi;

  1. Kitu gani kilitokea wakati Yesu anabatizwa

                 (a) Wingu jeusi

                  (b) Tetemeko la ardhi

                  (c) Mbingu za dunia zikamfunukia akaona Roho wa Mungu akishuka             
                 kama hua, akija juu yake, na sauti kutoka juu ikisema, Huyu ni
                 mwanagu mpendwa wangu, ninayependezwa naye

  2. Yesu alipopandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na ibilisi, alifunga kula siku ngapi?

                  (a) kumi

                  (b) Sita

                  (c) Arobaini
  3.   (i) Yesu alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, akimsihi akisema, Bwana mtumishi wangu amelala, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu akamwambia,

                  (a) Amini ameshapona

                  (b) Nitakuja, nimponye

                  (c) Nitakuja, nimuokoe na atapona.

    (ii) Yule akijibu akasema, Bwana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu, lakini sema neno na mtumishi wangu atapona. Yesu aliposikia hayo alistajabu akawambia wale waliomfuata

                  (a) Amini na wambie sijaona imani kubwa kama hii kwa yeyote
                 katika Israel

                  (b) Amini na wambie sijaona imani kubwa kama hii kwa yeyote
                 katika mkutano huu

                  (c) Amini na wambie sijaona upendo kubwa kama huu kwa yeyote
                 katika Israel

  4. (i) Kuna muujiza ambao Yesu aliufanya wa kuiongeza mikate na samaki ambapo wanafunzi wake walikula mpaka wakasaza. Ni mikate mingapi na samaki ngapi ambazo Yesu aliziombea kwa kutazama juu mbinguni kwa Mungu?

                  (a) Mikate miwili na samaki watano

                  (b) Samaki wawili na mikate mitano

                  (c) Mkate mmoja na samaki waili

    (ii) Masazo yaliyobaki baada ya wanafunzi kula na kushiba ilijaa vikapu vingapi?

                  (a) kumi na viwili

                  (b) Kuma na saba

                  (d) viwili

  5. Ni baada ya kufanya nini, Yesu aliwaambia, “Imeandikwa, nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala, bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi”.

                  (a) Ni baada ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na
                 kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
                 waliokuwa wanauzia njiwa

                  (b) Ni baada ya Yesu kuingia msikitini na kuona watu wakiuza na
                 kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
                 waliokuwa wanauzia njiwa

                  (c) Ni kabla ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na
                 kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
                 waliokuwa wanauzia njiwa
  6. (i) Yuda alipoona ya kuwa Ysu amekwisha kuhukumiwa, alifanya nini?

                  (a) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
                 vipande thelathini na moja vya fedha

                  (b) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
                 vipande thelathini vya fedha

                  (c) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
                 vipande thelathini vya dhahabu

    (ii) Ni maneno gani Yuda alisema baada ya kurudisha vile vipande alivyopewa kwaajili ya kumsaliti Yesu?

                  (a) Alisema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia
                  (b) Alisema, Sijakosea nilipoisaliti damu isiyo na hatia
                  (c) Alisema, Nalikosa nilipoisaliti damu iliyo na hatia

    (ii) Yuda baada ya kukimbia ndani ya hekalu kutokana na kumsaliti Yesu alifanya nini?

                  (a) Alikimbia na kujinyonga

                  (b) Alirudi na kumsujudia Yesu

                  (c) Alihuzunika sana na kulia

  7. Baada ya kusikia kuwa Herode amekufa Misri, Yusufu, Yesu na Bikira Maria  walitoka Israel ni wapi walienda kuishi?

                  (a) Nazareti

                  (b) Misri

                  (c) Marekani
  8. Taja majaribu matatu ambayo Yesu alijaribiwa na Ibilisi nyikani?

                  (a) (i) Mawe yawe mikate

                      (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu

                      (iii) Kumsujudia Ibilisi

                  (b) (i) Mchanga uwe mikate

                      (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha mlima

                      (iii) Kumsujudia Ibilisi

                  (c) (i) Mawe yawe mikate

                      (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu

                      (iii) Kumsujudia Mfalme
  9. Yesu aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. Na tazama akaja mtu mwenye ukoma, akamsujudia akisema,

                  (a) Bwana ukitaka unaweza kunitakasa

                  (b) Bwana ukitaka waweza kunibariki

                  (c) Bwana ukitaka waweza kunihurumia

  10. (i) Taja jina la mfalme aliyemfunga na kumtia Yohana Mbatizaji gereza?

                  (a) Kayafa

                  (b) Rulea Sanga

                  (c) Mfalme Herode

    (ii) Kwani Yohana alifungwa gerezani?

                  (a)  Yohana alimwambia sio halali kwa Herode kuwa na nduguye       
                 Filipo awe mke wake na Herode.

                  (b) Yohana alimwambia sio halali kwa Kayafa kuwa na nduguye
                 Musa awe mke wake na Herode.

                  (c) Majibu ya hapo juu sio sahihi

    (iii) Kwanini mfalme alipoona watu akaogopa kumuua Yohana Mbatizaji?

                  (a)  Yohana alimwambia sio halali kwa Herode kuwa na nduguye
                 Filipo awe mke wake na Herode.

                  (b) Kwasababu watu walimuona Yohana Mbatizaji kama Nabii

                  (c) Kwasababu watu walimuona Yohana Mbatizaji kama Mfalme

    (iv) Ni nani aliyecheza mbele ya Herode wakati wa sikuku yake ya kuzaliwa akampendeza Herode kwa uchezaji wake?

                  (a) Binti Herode

                  (b) Mjukuu wa Herode

                  (c) Rafiki yake na Binti Herode

    (v) Ni nani alimshauri huyu mtu aliyecheza mbele ya mfalme Herode na mpaka Herode akakubali kutimiza kiapo chake cha kumpa chochote atakachoomba?

                  (a) mama yake

                  (b) Kaka yake

                  (c) Rafiki yake

    (vi) Huyo aliyemfurahisha Herode kwa kucheza aliomba  nini apewe na huyo mfalme?

                  (a) hakuomba chochote

                  (b) aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji katika mfuko

                  (c) aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji katika kombe

    (vii) Unafikiri Herode alifuarahia ilo ombi la huyu aliyecheza vizuri katika sikuku yake ya kuzaliwa? Na kama alifurahi au alisikitika ni kwanini?

                  (a) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni aibu kwa watu waliokuwa
                 nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika sikukuu yake

                  (b) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni atakimbiwa na watu
                 waliokuwa nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika
                 sikukuu yake

                  (c) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni si haki na ni uonevu  kwa
                 watu waliokuwa nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika             
                 sikukuu yake

    (viii) Baada ya kichwa cha Yohana Mbatizaji kukatwa na kukabidhiwa yule kijana alicheza vizuri mbele ya mfalme Herode, ni wapi alikipeleka hicho kichwa?

                  (a) mama yake

                  (b) Kaka yake

                  (c) Rafiki yake


Monday, July 9, 2012

SHETANI ANYOHANGAISHA MIOYO YA WANADAMU

Mwandishi: Rulea Sanga

Ndugu zangu nyakati hizi ni za kumtafuta Mungu na kufanya kazi ya Mungu. Ulimwengu umeharibika, taarifa za kutisha na za kukatishana tamaa zimezidi. Watu wanaishi maisha ya hofu, hawana amani ndani ya maisha yao. Ndoto za ajabu zimewatala, zinawafanya waishi maisha ya wasiwasi. Binadamu wamekuwa wanyama, hawana huruma na wanapenda kuona wenzao wanateseka.

Wengine hawapendi hata kuona mwenzao anafanikiwa, wako tayari kutumia njia zozote kuhakikisha mambo yako yanaharibika. Imani za kishirikina zimetawala, watu wanalogana, watu wako tayari kupoteza maisha ya wenzao ili mradi mambo yao yanasonga mbele. Ukipita mitaani utakutana na vichaa wanahangaika na wengine wako uchi- hakuna wa kuwasitiri. Watoto na watu wazima wanachukuliwa misukule, wanafanyiwa mambo ya ajabu huko misituni na wachawi, vyakula vyao ni vya ajabu. 
 
Kuna baadhi ya watu wamezuiliwa milango yao ya mafanikio na ndugu zao au jamaa zao. Kila unapojitahidi kufanya jambo fualni, halifanikiwi. Wengine wanajitahidi kusoma kwa bidii, lakini wanapokuja kufanya mitahini ya mwisho wanafeli, ila ukiangalia maendeleo yao kabla ya mitihani yalikuwa mazuri sana. Kuna wengine wamelogwa na kusemewa maneno mabaya na wabaya ya kuwa kila jambo utakalofanya hutafanikwa, nah ii imetawala sana katika kipindi hiki.

Wachawi wanawaloga watu na kuwatupia majini na kuwasemea maneno mabaya. Utaona msichana ni mrembo sana na amefanikiwa kimaisha lakini hapati mtu wa kumuoa. Wasichana kama hawa wanafikia hatua hata ya kuwa wabaya katika jamii na kuona kama wametengwa na ulimwengu. Wanatamani kufanya vitendo viovu na kudiriki kuingia katika ushiriana ili wapate waume. Na hili sio tu kwa wasichana bali hata kwa wanaume ambao nao hujiingiza katika mambo maovu ya ushoga, ushirikina, ulevi, utekaji, uchawi, wizi na mambo mengine kama hayo.

Barabarani lusambazwa nuksi za kila aina, ajali zimetawala. Wachawi wanaweka mambo yao ya ajabu katika barabara ili kusababisha ajali, na ajali inapotokea wao hufurahia kwani kwao damu ma myama ya watu ndio chakula chao kikuu na ndicho kinachowasaidia kufanikiwa mambo yao. Hili ni ja,bo la kusikitisha sana na linaumiza sana hasa pale unaposikia ndugu yako amepoteza maisha kwa jajali mbaya.

Vita ndani ya familia zimetawala sana katika ulimwengu huu, kuna baadhi ya familia hazielewani, utaona mama na mototo wake wanatukana na kushikiana visu ili wauane. Shetani ametawala katika familia zetu. Hapendi kuona wewe unaelewana na ndugu yako. Anajitahidi kutumia mbinu zake kuhakikisha hakuna amani katika familia yako. Cha kushangaza utaona pengine katika familia kuna wengine wamefanikiwa kiuchumi na nimatajiri sana, lakini ndani ya hiyo familia kuna maskini wakutupwa na hakuna wakuwasaidia. Shetani mara nyingine anaweza kukuzuia wewe kutokuwa na moyo wa kusaidia jamii yako, au anaweza kuzuia wewe maskini kuonekana hufai kwa yule ndugu yako aliyefanikiwa

Wasomi wengi wamesoma lakini wanakosa kazi, kila wakienda kuomba kazi hawafanikiwi. Kuna baadhi ya ofisi ukipeleka vyeti vyako na wakiona wewe umesoma sana wanakataa kukupa kazi eti kwasababu umesoma sana na hawataweza kukulipa mshahara kulingana na elimu yako. Shetani ni majanja sana na ni mjinga, huwapa wajiri kipofu cha kufikiri na kuwadanganya kwa kuwapa “statement” ambayo ni ya kipimbavu ya kuwafukuza wasomi wazuri ambao wangeweza kuinua kampuni. Baadhi ya wasomi wengine hawaangalii sana kiwango cha msharaha ila wanachotaka na “experience” tu ya kazi.

Shetani hana huruma kwa wanadamu, kuna baadhi ya watu wamelogwa kuwafanya mazezeta, wengine chakula chao ni mikaa ya moto, barafu, kinyesi, mikojo, michanga, kucha, na vitu ambavyo mwanadamu hawezi kuvila. Furaha yake ni kuona unateseka na hufanikiwi kwa lolote. 
 
Ombi langu kwako unayeteseka, jaribu kuwa karibu sana na Mungu kwa kufanya mapenzi yake mema. Pia kuwa na imani kwa kila jambo unaloomba kwa Mungu kuwa linaenda kufanyika. Kumkemea shetani kuwe ni moja ya kazi yako ya kila siku. Maombi yasipungue katika kinywa chako. Na unapoomba umaanishe na usiweke kama ratiba fulani. Maombi yako yawe silaha katika kupambana na adui shetani. Tafuta watu waliokoka kabisa na anza kushirikiana nao katika kusoma biblia na kuijadili ili kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na Mungu. Epukana na wanaokukatisha tamaa kuhusu Mungu. Ukiwa na Mungu utapambana na watu wengi ambayo watakukatisha tamaa, na huyo ni shetani kwani shetani mara zingine anatumia watu au rafiki au ndugu zako na kukuletea habari mbaya kuhusu Mungu.
 
Mungu wangu akubariki






Monday, July 2, 2012

PADRI AAMURU KABURI KUFUKIWA, AGOMA KUMZIKA MUFU KWA SABABU ALIACHA KUSALI

KATIKA hali isiyotarajiwa, Padri wa Kanisa Katholiki Jimbo la Sumbawanga , Evalin Kombe hivi karibuni aliamuru kufukiwa kwa kaburi lililokuwa tayari kuhifadhi mwili wa mmoja wa waumini wa kanisa hilo kwa dai kuwa muumini huyo alikuwa ameacha kusali.
Mbali ya kuacha kusali, Padri huyo pia alidai sababu nyingine ya kuzuia mwili wa marehemu usizikwe katika makaburi hayo, wakati wa uhai wake, alikuwa anaishi na mume bila kufunga ndoa kanisani.

Kitendo cha Padri huyo ambaye ni Paroko wa Kanisa la Pito lililopo kijijini kuzuia mwili wa marehemu Noelia Mwanisenga (29) asizikwe kwenye shamba hilo la wafu kulichelewesha maziko ya marehemu kwa zaidi ya saa tatu .
Akisimulia kisa hicho, mume wa marehemu Noelia, Boniface Sali (32), mkazi wa kijiji cha Tamasenga ambaye pia ni askari Mgambo alisema kuwa wakati wakijiandaa na maziko wachimba kaburi ghafla walirejea msibani Pito na kutoa taarifa kuwa Paroko ameamuru kaburi lifukiwe na kuwa marehemu wake hatazikwa katika shamba hilo la wafu.
Alisema baada ya majadiliano wafiwa walifikia uamuzi wa kuchimba kaburi jingine kijiji jirani cha Tamsenga na kumsitiri marehemu wao jioni tena bila ibada zinazohusu imani yake ya Kikatholiki aliyokufa nayo.

Sali alikiri kuwa yeye ni mlokole wa madhehebu ya Pentekoste na marehemu mkewe alikuwa muumini wa Kanisa Katholiki.
Ignas Mwanisenga ambaye alishiriki kuchimba kaburi la marehemu kijijini Pito anadai kuwa Padri Kombe alipofika makaburini alikuta wanamalizia kuchimba kaburi hilo na kuwataka kulifukia huku akiwatishia kuwa kama angekuwa na bunduki angeweza kuwaua.
“Alionekana kuwa na hasira kwani alitutishia kuwa kama angekuwa na bunduki angetuua, kwanza alifukia mwenyewe halafu alituachia sisi tutufukie kusimamia zoezi hilo mpaka tukalimaliza huku akisisitiza kuwa kama tungeshindwa angefukia yeye mwenyewe hata kama ingemchukua siku kadhaa kufanya hivyo” alisema Ignas .

Sali alisema yeye na mkewe ambaye alikuwa askari Mgambo waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka minane na kujaliwa kupata watoto watatu na wiki mbili zilizopita aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Charles Kusula , Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Tamasenga alithibitisha kuwa marehemu Noelia alizikwa kijijini humo saa 12 jioni .
Tukio hilo ambalo limetokea wiki mbili zilizopita, si la kwanza, kwani Padri huyo alishawahi kukataa kumzika katika makaburi hayo ya Pito, Marehemu Steven Kipesha (34), hali iliyomlazimu baba mdogo wa marehemu, Oto Kipesha mkazi wa Kijiji hicho cha Pito kumzika marehemu upenuni mwa nyumba yake.
Kutokana na kitendo cha Padri Kombe kufukia kaburi, ndugu wa karibu wa marehemu huyo na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Pito na vijiji jirani wamelielezea tukio hilo kuwa ni mkosi kwa wafiwa.
Baadhi ya wazee wa jadi waliozungumza na mwandishi wa habari hii wanadai kitendo cha Padri huyo kinaashiria mkosi kijijini humo wakisema kufukia kaburi tupu kutasababisha balaa jingine la kifo katika familia hiyo iliyozuiwa kumzika marehemu wao kaburini humo na kwenda kumzika kwingineko.

“Sisi katika desturi yetu ya kimila iwapo kaburi tayari limeshachimbwa lakini baadaye maamuzi yakatolewa marehemu asizikwe humo, basi hukatwa mgomba na ‘kuzikwa‘ kaburini , ikiwa ni njia ya kuondoa mkosi kwa wafiwa, lakini si kufukia kaburi likiwa tupu,” alisema mmoja wa wazee hao wa jadi ambaye hakuwa tayari jina lake liandikwe gazetini.
“Kwa kawaida tunavyofahamu sisi ni kwamba kama uamuzi umeshatolewa kuwa marehemu hatazikwa katika kaburi lililokwishaandaliwa kwa ajili yake basi kamwe kaburi hilo huwa halifukiwi, huachwa hivyo hivyo likiwa wazi na tupu lakini kitendo hiki cha Padri kufukia kaburi sio tu kimetustaajabisha wengi bali pia ni machukizo kwetu,” alisema Afred Mwananzumi , baba mdogo wa marehemu.

Naye mkazi mwingine wa kijiji hicho cha Pito Oto Kipesha alimweleza mwandishi wa habari hizi kijijini humo jana kuwa alifikia maamuzi ya kumzika Steven Kipesha (34) ambaye ni mtoto wa kaka yake upenuni mwa nyumba yao kijijini humo baada ya Padri Kombe kuwazuia wasimzike marehemu huyo katika shamba la wafu kijijini humo kwa madai kuwa aliacha kusali muda mrefu.
“Marehemu alihamia Tunduma miezi mitatu iliyopita na baadaye aliugua na kufariki dunia katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya tulipopata taarifa za msiba tulijiandaa na kuusafirisha mwili hadi kijijini hapa lakini Paroko Kombe alituzuia tusimzike katika shamba la wafu kijijini hapa kwa kuwa eti alikuwa hasali …… mie nikachukua uamuzi wa kumzika upenuni mwa nyumba yangu.
Alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na visa hivyo viwili akiwa ofisini kwake jana katika Parokia ya Kanisa Katholiki kijijini Pito , Padri Kombe alikiri kuwa aliwaamuru vijana aliowakuta wakichimba kaburi katika shamba la wafu kijijini humo walifukie hata hivyo alikanusha kuwatolea maneno ya vitisho kuwa kama angekuwa na bunduki basi angewaua.
Akieleza sababu za kuchukua uamuzi wake huo , Padri Kombe alisema kuwa visa vya aina hiyo vimekuwa vikitokea sio kijijini humo pekee bali na kwingineko kwamba kidesturi zipo aina tatu za maziko katika Kanisa Katholiki ambapo marehemu wote wawili Kipesha na Noelia waliangukia katika aina ya tatu .
Alisema aina hiyo ya tatu inatokea pale muumini pamoja na kwamba amebatizwa, lakini hasali hivyo anajirudisha katika upagani basi azikwe mahali popote pale lakini sio katika shamba la wafu la Kanisa.

“Mara nyingi nimekuwa nikiwaeleza haya tena huwa nawafafanulia kuwa kwa kuwa hawataki kuja kanisani kusali basi wakifa wazikwe huko huko majumbani mwao kwa kuwa ni mahali wanapopapenda zaidi kwanini wasumbuliwe kupelekwa mahala pengine kwa maziko? “ Alihoji.
Pia aliendelea kufafanua akisema aina ya kwanza ya maziko inayofuatwa na Kanisa hilo Katholiki inahusu waumini waliobatizwa ambao katika uhai wao waliweza kutimiza na kuishi katika Ukatholiki wakisali na kushiriki mambo yote ya kanisa.
Padri Kombe alisema maamuzi hayo ya kutowazika katika shamba la wafu ni fundisho kwa wengine ili wafuate ibada kama watapenda kushughulikiwa kiimani baada ya kifo.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Sunday, July 1, 2012

TUJIKUMBUSHE NA KILE KILICHOTUPIWA NA SAMSASALI KATIKA BLOG


Chini Ya Carpet......TB Joshua Kutua Tanzania??

Pichani ni Mtumishi wa Mungu kutoka Tanzania na kiongozi wa Kanisa la Ephata akiwa na Nabii TB Joshua nchini Nigeria mwaka 2009. Mtumishi Mwingira alifanya Ziara nchini humo na kuhudhuria Africa Apostoric Forum iliyofanyika nchini humo.


Baada ya Jitihada za Miaka ya Nyuma Kushindikana za Kumleta Mtumishi wa Mungu TB Joshua hapa Tanzania huenda mtumishi huyo akakanyaga ardhi ya Tanzania.


Chanzo Cha habari kilikataa kutaja nani na nani wanafanya mpango wa kumleta na lini na wapi ila alisema "Unakumbuka siku za nyuma ilikuwa Nabii TB Joshua aje na alisha ridhia mwaliko ule uliokuwa unaratibiwa na Mtumishi wa Mungu Apostle.............(Jina tunalo) na alishakubali ila Roho akaelekeza tofauti, basi mazungumzo yameanza tena, sababu imekuwa na support kubwa zaidi" mwisho wa kunukuu taarifa hiyo.


Blog ilipotaka kujua lini na wapi na nani ana organize chanzo kilisema "Mambo yakiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani"


NINI KIFANYIKE ILI KUDHIBITI UHARAMIA WA KAZI ZA WASANII NCHINI ILI KUHAKIKISHA WAHUSIKA WANAFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA NA KUCHUKULIWA HATUA STAHIKI KAMA MAJAMBAZI WENGINE


Pamoja na serikali kuahidi kwamba juhudi zinachukuliwa ili kuleta heshima na thamani ya wasanii na kazi zao nchini, lakini kinyume chake hivi sasa kazi feki zimezagaa hadi vichochoroni.

Pamoja na wasanii kujinyima, kukopa, na kuangaika hapa na pale ili kuweza kuandaa kazi zao zinazogharimu mamilioni ya pesa lakini watu wanazitumia bila kutoa jasho lolote, tena wanaziuza bei chee. Hili ni janga, huu ni msiba mkubwa kwa wasanii nchini.

Uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu umebaini kuwapo kwa kundi kubwa la wafanyabiashara wanaouza kazi za Wasanii mbalimbali zilizodurufiwa (duplicated) kwa bei ya chini na kusababisha wasanii kutofaidika na kazi zao.

Nani awafute machozi wasanii, nani alete matumaini kwa wasanii? Nani atuondolee mtandao huu wa maharamia wa kazi za wasanii?

Ikiwa malaria haikubaliki, na uharamia huu haukubaliki.

Chama cha muziki wa injili nchini (CHAMUITA) kinapinga tabia hii
Kazi feki zikitayarishwa kuchomwa huko China

HERE IS THE AUTOBIOGRAPHY OF TB JOSHUA

(This man is real unique,i real admire his humility and true love-Author)


God chooses grace rather than works”(Ephesians 2:8-9)
This means that if the weak come to Him, He would help their weakness just as He would help the strong. God knows we are weak – that is why He chooses grace. If God had chosen works rather than grace, man would have the autonomy to choose whom to help with his works and how to do His works.
The battle would be for the strongest leaving no room for people like me (T.B. Joshua). The race would be for the swiftest leaving no room for people like me (T.B. Joshua).”
Isaiah 6:8 – “Then I heard the voice of the Lord saying, “Whom shall I send? And who will go for us?” And I said, “Here am I. Send me!”
T.B. Joshua is just one of those who have submitted to the will of God. He acknowledges that if God had chosen works rather than grace, no one would merit His mercy.
In a sermon titled, “By His Grace”, he explained:“Wisdom in the practical sense of ability and skill cannot guarantee success in life. It is the goodness of our cause that interests God more than physical and mental disposition. This explains why the weak people like me who are without great strength, a smooth tongue, fast legs or high learning should ever remain grateful to God”.
Right from the outset of his incredible journey, the hand of God has been clearly evident in the life of Prophet T.B. Joshua. He was born on June 12th, 1963 in the small village of Arigidi in Akoko, Ondo State, Nigeria. The pregnancy period of his mother was by no means ordinary, as the baby remained in her womb for 15 months before he was born. Significantly, almost a hundred years prior to his birth, it had been prophesied that a young man would emerge from the poor Oosin quarters and that God would use him mightily. Another remarkable event occurred when he was three days old, as a large boulder crashed through the roof of his house, missing the baby by mere inches. This incident led to his mother naming him, ‘Temitope’, meaning, ‘What You (God) have done for me is worthy of thanks’.
During his elementary education at St. Stephen’s Anglican primary school, Arigidi, he was the leader of the Student Christian fellowship. He was the smallest in the class but led the prayer during the school devotions and was known as ‘small pastor’. He was unable to complete his secondary education due to poverty.
Reflecting on his early life, he said: “I found myself in a family background that irritated me. My natural circumstance of birth was poverty. I come from a very humble background. Poverty loomed large in the family. The little education I had was through self-effort. I know many people with a similar circumstance of birth who did otherwise. They allowed their circumstance to influence their will. Their dreams crashed on the rocks of disappointment, failure and setback …In those early years of my life, we knew we would be blamed for what we gave our attention to.”
In an article written by T.B. Joshua himself, titled, ‘Everything Big Starts Little’, he explains more…
Very early in life, he knew how much he needed God, so he did not allow the situation around him to affect his relationship with God. As described in his own words, T.B. Joshua recounts how he discovered the direction of God’s calling for his life:

Sarah Shilla Kutoka na "Let It Rain, In His Presence"

Mwanamuziki anayekuja Juu katika Gospel Music, The Sarah Shilla siku ya Tarehe 5 August, 2012 Anatarajia ku "Launch" Albam Yake yenye Jina la "Let It Rain In His Presence"

Blog itazidi Kukupa Details za Tukio Zima Linavyokwenda.



VANYASANGA POST TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...