Wednesday, June 27, 2012

MCHUNGAJI BURTON SANGA  NAPENDA KUWASHUKURU WOTE WALIHUSIKA KATIKA MSIBA WA MAMA YANGU MPENDWA AMBANGILE SANGA.

Shukrani zangu za dhati kwawale  wote waliokuwa pamoja nasi katika kumuuguza mama yangu alipokuwa hospitali ya Chimala Mbeya. Tunashukuru kwa kunifariji, kunichangia,kunitia moyo na maombi hasa pale mama alipokuwa amelazwa hospitalini.

Mbali na hapo ninawashukuru madaktari wote waliokuwa nami bega kwa bega kwa kumtibu mama yangu. Na pia namshukuru sana Dk. Mahenge kwa kujitoa nasi katika shughuli zote, tangia mama alipokuwa hospitalini mpaka anatoweka duniani. MUNGU AKUZIDISHIE PALE ULIPOTOA.

Napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa wote waliohudhuria katika mazishi ya mama yangu yaliyofanyika katika makaburi ya Itoroha Uyole Mbeya siku ya jumamosi 23 Juni 2012 pamoja na wachungaji wote, MUNGU WANGU NINAYEMTUMIKIA AWABARIKI.

Wenu katika Bwana
 MCH. BURTON SANGA


No comments:

Post a Comment

VANYASANGA POST TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...