Wednesday, June 27, 2012

MSIBA ULIOMKUMBA BLOGGER WENU WA RUMAAFRICA, RULEA SANGA ALIPOFIWA NA MAMA YAKE MZAZI AMBANGILE LANZON SANGA
Hii ni siku ambayo siwezi kuisahau pale nilipompoteza mama yangu mzazi katika hospitali ya Chimala Mbeya siku ya ya Jumamosi 22 Juni 2012. Mama yangu alipata ugonjwa wa ghafla pale alipoaanza kutapika na baadae kukimbizwa dispensary na baada ya kupimwa aligundulika ana malaria mbili. Mama alirudishwa nyumbani na baada ya hapo usiku wake mama yangu hali iliaanza kubadilika na kuishiwa nguvu. Hali hiyo ilizidi kuwa mbaya na baadae kaka yangu Burton Sanga aliamua kukimbiza hospitali ya Chimala iliyoko Mbeya. Mama aliaendelea na matibabu na baadae kugundulika kuwa alikuwa na Blood Pressure (BP) na baada ya siku kama mbili aligundulika kuwa anaumwa Kisukari. Siku tatu baadae hali ya mama yangu ilikuwa mbaya sana.
Mama aliwekewa mpira ya Oxygen na mrija wa kupitisha chakula. Mama hakuweza kuongea kwa muda wote aliokuwa hospitali, lakini namshukuru sana Mungu wangu, baada ya kuniona mama alicheka kicheko cha maumivu na kuniambia "Mwanangu umekuja kuniuguza???" Nililia sana kumuona mama anavyoteseka na kuhema, kwani alikuwa anasumbuliwa sana na utoaji na uingizaji oxygen. Pia alikuwa analalamika na maumivu aliyokuwa anapata kutokana na kulalia mgongo kwa muda mrefu.
Siku ya Jumatano mama yangu hakuweza kuongea kitu chochote, macho yake yalikuwa yamefumba na mdomo wake ulikuwa umeachama kwaajili ya hewa. Mama alipochomwa na sindano na daktari kama nne begani hakuweza kushtuka wala kuhisi maumivu yote. Ndugu zangu walipokuwa wanatoa nguo zake mama alikuwa bado kafumba macho yake na hakuonyesha sign ya kuumia.
 
Nakumbuka kabla ya kifo cha mama yangu, ilikuwa ni siku ya Alhmaisi nilipomuombea sana mama yangu na kuwaaga baadhi ya ndugu zangu kuwa nataka niende Dar es Salaam kufuatilia pesa ambazo zitasaidia katika matibabu na siku ya jumatatu nitarudi tena Mbeya kuumuuguza mama yangu, lakini haikuwezekana. Ilipofika siku ya Ijumaa nilienda hospitalini kwaajili ya kumuaga mama yangu na ndugu zangu kuwa naenda Dar.
Nilipofika hospitalini nilikutana na shemeji yangu mke na kaka yangu Mchungaji Burton Sanga, alinikimbilia na kuniuliza "begi lako liko wapi?" na mimi nilimjibu "nimeliacha hotelini"  aliniangalia kwa huruma sana, na mimi nikaona baadhi ya ndugu zangu wako katika chumba cha kuhifadhia maiti. Shemeji aliniambia "Jipe moyo mama hayupo tena duniani" nililia sana kwa maana sikuamini kwani siku ya jana yake nilimuombea na kumshika mkono, kumbe ilikuwa ndio alama ya kuaagana 
Nilimshika mama yangu mkono kwa mara ya mwisho na usiku wa ijumaa mama aliaga dunia.
Siku ya Ijumaa ya 22 Juni 2012 mida ya saa 4:30am mama aliaga dunia, na sasa amepumzika katika makaburi yaliyoko Mbeya uyole kama unaelekea Tukuyu.
Mama ameacha watoto wanne, Yohana Sanga, Fidness Sanga, Burton Sanga na Rulea Sanga.
Blogger wenu nawaashukuru sana wale wote walionitumia pesa kwa kupitia Tigo Pesa kama rambirambi na maneno ya faraja ambayo yalinifariji sana. MUNGU WANGU ATAWALIPA
Ngoja tuone Safari nzima ilivyokuwa:

NIKIWA SAFARINI KUELEKEA MBEYA
 Nikiwa maeneo ya Morogoro
 Mishika ndicho kilikuwa chakula changu siku hiyo
Nikisubiri safari kuanza kuelekea Mbeya

MAMA AKIWA KATIKA HOSPITALI YA CHIMALA MBEYA
Mama yangu ambangile Lanzon Sanga akiwa amelazwa hospitalini Chimala Mbeya siku ya Jumamosi
 Kutoka kushoto ni wauguzi, dada yangu Aulelia Mahenge mtoto wa mama mkubwa, Binamu yangu, Mama Simda
 Shemeji yangu ambaye ni mke na kaka yangu Mchungaji Burton Sanga, Mama Judy.
Mama Judy amemlea mama yangu kwa muda wa miaka 17 tangia atoke Iringa na mpaka mauti imemchukua
Dada yangu Fidness Sanga akimwangalia mama 
 Blogger wenu Rulea Sanga (kulia) nikimtakia afya njema mama yangu

Daktari akimtibu mama yangu, pembeni ni shemeji yangu, mke na kaka yngu marehemu Amir Sanga a.k.a Short
 Daktari akiwa na baadhi ya ndugu na jamaa
PICHA BADO ZINAKUJA

No comments:

Post a Comment

VANYASANGA POST TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...