Sunday, July 1, 2012

NINI KIFANYIKE ILI KUDHIBITI UHARAMIA WA KAZI ZA WASANII NCHINI ILI KUHAKIKISHA WAHUSIKA WANAFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA NA KUCHUKULIWA HATUA STAHIKI KAMA MAJAMBAZI WENGINE


Pamoja na serikali kuahidi kwamba juhudi zinachukuliwa ili kuleta heshima na thamani ya wasanii na kazi zao nchini, lakini kinyume chake hivi sasa kazi feki zimezagaa hadi vichochoroni.

Pamoja na wasanii kujinyima, kukopa, na kuangaika hapa na pale ili kuweza kuandaa kazi zao zinazogharimu mamilioni ya pesa lakini watu wanazitumia bila kutoa jasho lolote, tena wanaziuza bei chee. Hili ni janga, huu ni msiba mkubwa kwa wasanii nchini.

Uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu umebaini kuwapo kwa kundi kubwa la wafanyabiashara wanaouza kazi za Wasanii mbalimbali zilizodurufiwa (duplicated) kwa bei ya chini na kusababisha wasanii kutofaidika na kazi zao.

Nani awafute machozi wasanii, nani alete matumaini kwa wasanii? Nani atuondolee mtandao huu wa maharamia wa kazi za wasanii?

Ikiwa malaria haikubaliki, na uharamia huu haukubaliki.

Chama cha muziki wa injili nchini (CHAMUITA) kinapinga tabia hii
Kazi feki zikitayarishwa kuchomwa huko China

No comments:

Post a Comment

VANYASANGA POST TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...