Sunday, July 1, 2012

TUJIKUMBUSHE NA KILE KILICHOTUPIWA NA SAMSASALI KATIKA BLOG


Chini Ya Carpet......TB Joshua Kutua Tanzania??

Pichani ni Mtumishi wa Mungu kutoka Tanzania na kiongozi wa Kanisa la Ephata akiwa na Nabii TB Joshua nchini Nigeria mwaka 2009. Mtumishi Mwingira alifanya Ziara nchini humo na kuhudhuria Africa Apostoric Forum iliyofanyika nchini humo.


Baada ya Jitihada za Miaka ya Nyuma Kushindikana za Kumleta Mtumishi wa Mungu TB Joshua hapa Tanzania huenda mtumishi huyo akakanyaga ardhi ya Tanzania.


Chanzo Cha habari kilikataa kutaja nani na nani wanafanya mpango wa kumleta na lini na wapi ila alisema "Unakumbuka siku za nyuma ilikuwa Nabii TB Joshua aje na alisha ridhia mwaliko ule uliokuwa unaratibiwa na Mtumishi wa Mungu Apostle.............(Jina tunalo) na alishakubali ila Roho akaelekeza tofauti, basi mazungumzo yameanza tena, sababu imekuwa na support kubwa zaidi" mwisho wa kunukuu taarifa hiyo.


Blog ilipotaka kujua lini na wapi na nani ana organize chanzo kilisema "Mambo yakiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani"


No comments:

Post a Comment

VANYASANGA POST TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...